عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما: عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ نَهَى عَنِ النَّذْرِ، وَقَالَ: «إِنَّهُ لَا يَأْتِي بِخَيْرٍ، وَإِنَّمَا يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنَ الْبَخِيلِ».
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka nadhiri, nayo ni mtu kujiwajibishia kitu ambacho sheria haijamlazimisha kukifanya, na akasema kuwa: Nadhiri haiwahishi kitu na wala haikicheleweshi, bali hutolewa vilivyo kwa mtu bahili ambaye hafanyi ila yale ya wajibu pekee, nakuwa nadhiri haileti kitu ambacho hakikukadiriwa.
Mafunzo
- Nadhiri si sheria, lakini akiweka nadhiri ni lazima kwake kuitekeleza kama haitokuwa ya maasi.
- Sababu ya kuikataza nikuwa (haiji kwa heri); kwa sababu hairejeshi chochote katika kadari za Mwenyezi Mungu; na ili asidhanie mtia nadhiri kuwa kutimia kwa ombi lake kulikuwa kwa sababu ya nadhiri, na Mwenyezi Mungu hana haja na hilo.
- Amesema Al-Qurtubi: Makatazo haya mahali pake ni mtu kusema, kwa mfano: Ikiwa Mwenyezi Mungu atamponya mgonjwa wangu, basi nitatoa sadaka kadhaa, lengo lililotajwa hapo juu kuwa ni karaha kufanya hivyo ni kwa sababu alipoweka nia ya utoaji wake ni mpaka litimie lengo fulani, ikaonyesha wazi kuwa hakuwa na nia ya kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyafanya, bali ametumia njia ambayo ndani yake kuna kubadilishana, na kinacholiunga mkono hili nikuwa lau mgonjwa wake asingepona basi asingetoa sadaka kwa sababu alichokitoa kakiambatanisha na kupona kwake, na hii ni hali ya bakhili, kwani hatoi chochote katika pesa yake isipokuwa kwa kutaka badala ya haraka ya kile alichokitoa kwa kawaida.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 124) (6608).
صحيح مسلم (3/ 1261) (1639).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص353).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص693).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي رَهْطٍ مِنَ الأَشْعَرِيِّينَ أَسْتَحْمِلُهُ، فَقَالَ: «وَاللَّهِ لاَ أَحْمِلُكُمْ، مَا عِنْدِي مَا أَحْمِلُكُمْ» ثُمَّ لَبِثْنَا مَا شَاءَ اللَّهُ فَأُتِيَ بِإِبِلٍ، فَأَمَرَ لَنَا بِثَلاَثَةِ ذَوْدٍ، فَلَمَّا انْطَلَقْنَا قَالَ بَعْضُنَا لِبَعْضٍ: لاَ يُبَارِكُ اللَّهُ لَنَا، أَتَيْنَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَسْتَحْمِلُهُ فَحَلَفَ أَنْ لاَ يَحْمِلَنَا فَحَمَلَنَا، فَقَالَ أَبُو مُوسَى: فَأَتَيْنَا النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرْنَا ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: «مَا أَنَا حَمَلْتُكُمْ، بَلِ اللَّهُ حَمَلَكُمْ، إِنِّي وَاللَّهِ -إِنْ شَاءَ اللَّهُ- لا أَحْلِفُ عَلَى يَمِينٍ، فَأَرَى غَيْرَهَا خَيْرًا مِنْهَا، إِلَّا كَفَّرْتُ عَنْ يَمِينِي، وَأَتَيْتُ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ».
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na kundi la Ash’ari ili kumuomba atuchukue, akasema: “Wallahi sitokuwa na chochote cha kukubebeni ” Kisha tukakaa muda kidogo aliopenda Mwenyezi Mungu tukae, tukaletewa ngamia, akaamrisha tupewe wanyama watatu kwa ajili yetu, tulipoondoka wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: Mwenyezi Mungu hatotubariki, tumemuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamuomba atubebe katika vipando lakini akaapa kuwa hatotubeba, kisha akatubeba, akasema Abuu Musa: Basi tukaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamueleza hilo, akasema: “Si mimi niliyekubebeni, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekubebeni Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anasimulia Abuu Musa Al-Ash’ari radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akiwa na kundi la kabila lake, na makusudio yao yalikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ili awape ngamia wapande, ili kuweza kushiriki katika jihadi, aliapa rehema na amani ziwe juu yake kuwa hatowabeba, na hakuwa hana chochote cha kuwabeba, basi wakarudi na kukaa kwa muda, kisha wakaletewa ngamia watatu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawatumia wale mabwana, baadhi yao wakaambiana: Mwenyezi Mungu asitubariki kwa ngamia hawa; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliapa kutotubeba, basi wakamjia na wakamuuliza, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Aliyekubebeni ni Mwenyezi Mungu Mtukufu; Kwa sababu yeye ndiye aliyetoa ufanikishaji na akaruzuku, lakini mimi ni sababu ya haya kutokea kupitia mikono yangu, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wallahi, akipenda Mwenyezi Mungu, sitaapa kufanya au kuacha chochote, na nikaona kuwa kisichokuwa kiapo hicho ni heri na bora zaidi, isipokuwa nitafanya lililo bora zaidi, na kuyaacha niliyoapa, na ninalipa kafara ya kiapo changu.
Mafunzo
- Inafaa kuapa bila kutakwa kuapa; ili kuitia mkazo habari hata kama ni ya jambo la baadae.
- Inajuzu kutojipa uhakika kwa kusema “Mwenyezi Mungu akipenda” baada ya kiapo, ikiwa kutafanywa kwa nia na kiapo na kukaunganishwa nacho, basi kafara haitohitajika kwa mwenye kuvunja kiapo chake.
- Himizo la kuvunja kiapo ikiwa ataona jambo bora kuliko hilo, na atatoa kafara ya kiapo chake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 146) (6718).
صحيح مسلم (3/ 1268) (1649).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص345).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص682).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ وَهُوَ فِيهَا فَاجِرٌ لِيَقْتَطِعَ بِهَا مَالَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ، لَقِيَ اللَّهَ وَهُوَ عَلَيْهِ غَضْبَانُ». قَالَ: فَقَالَ الْأَشْعَثُ: فِيَّ وَاللَّهِ كَانَ ذَلِكَ؛ كَانَ بَيْنِي وَبَيْنَ رَجُلٍ مِنَ الْيَهُودِ أَرْضٌ، فَجَحَدَنِي، فَقَدَّمْتُهُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلَكَ بَيِّنَةٌ؟» قُلْتُ: لَا. قَالَ: فَقَالَ لِلْيَهُودِيِّ: «احْلِفْ». قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِذَنْ يَحْلِفَ وَيَذْهَبَ بِمَالِي. فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: {إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا}. إِلَى آخِرِ الْآيَةِ.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia". Akasema: Akasema Al-Ash'athi: Kwangu mimi Wallahi kulitokea tukio hilo; kulikuwa na Ardhi baina yangu na bwana mmoja Yahudi, akanipinga kuwa si yangu, nikampeleka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuniambia: "Je una ushahidi?" Nikasema: Hapana: Akasema kumwambia Yahudi: "Toa kiapo". Anasema: Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sasa si ataapa na atachukua mali yangu!. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo..." mpaka mwisho wa aya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoa kiapo kwa Mwenyezi Mungu huku muapaji akijua kuwa anaapia uongo ndani yake, ili ajipatie kwa kiapo hiki mali ya mwenzake; huyu atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia, akaeleza Ash'athi bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilisema hilo wakati ambao kulikuwa na mzozo kati yake yeye na bwana mmoja Yahudi katika umiliki wa Ardhi, wakashitakiana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia Ash'athi: Unatakiwa kuleta ushahidi ili kuthibitisha madai yako, ukishindwa kuuleta basi hutokuwa na haki zaidi ya kiapo cha hasimu wako mshitakiwa, Ash'athi akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, basi huyu bwana Yahudi si ataapa pasina hofu na mali yangu itapotea, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kusadikisha hilo ndani ya Qur'ani kauli yake Mtukufu: "Hakika wale wanaouza" na wanabadilisha "ahadi ya Mwenyezi Mungu", na usia wake kwa waumini kwa kutimiza amana "na viapo vyao" na viapo vyao kwa jina lake kwa uongo "kwa thamani ndogo" kwa starehe za dunia "Hao hawana fungu lolote kwao Akhera" wala sehemu "Wala hatowasemesha Mwenyezi Mungu", kwa maneno yanayowafurahisha na kuwanufaisha, bali atawaghadhibikia, "wala hatowatazama siku ya Kiyama", mtazamo wa huruma na wema, "wala hatowatakasa" kwa kuwasifia kwa mazuri, wala hatowasafisha kwa kuwapa msamaha wa madhambi na machafu "na watakuwa na adhabu chungu" yenye kuumiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya.
Mafunzo
- Uharamu wa kuhalalisha mali za watu kwa dhulma.
- Uzito wa haki za waislamu katika kidogo na kingi.
- Ushahidi kwa mwenye kudai, na kiapo kwa mlalamikiwa atakapokataa.
- Haki inathibiti kwa mashahidi wawili, usipopatikana ushahidi kwa mlalamikaji, basi ni lazima kwa mlalamikiwa kutoa kiapo.
- Uharamu wa kiapo cha (kuzama) nacho ni kiapo cha uongo ambacho muapaji anajikatia haki ya mtu mwingine, nalo ni katika madhambi makubwa, ambalo linamtia mtu katika ghadhabu za Mwenyezi Mungu Mtukufu na adhabu zake.
- Nasaha za hakimu wakati wa mzozo, hasa hasa wakati wa kutaka kiapo.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 121) (2416).
صحيح مسلم (1/ 123) (138).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 136).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص687).
فتاوى اللجنة الدائمة - اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء (23/ 513).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن ثابِت بْن الضَّحَاكِ رضي الله عنه أنه بايع رسول الله صلى الله عليه وسلم تحت الشجرة، وأن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «من حلف على يمين بملة غير الإسلام، كاذبا مُتَعَمِّدًا فهو كما قال، ومن قتل نفسه بشيء عُذِّبَ به يوم القيامة، وليس على رجل نَذْرٌ فيما لا يملك» وَفِي رِوَايَة: «ولَعْنُ المؤمنِ كَقَتْلِهِ». وفي رواية: «من ادَّعَى دَعْوَى كَاذِبَةً لِيَتَكَثَّرَ بها لم يَزِدْهُ اللهُ -عزَّ وجل- إلا قِلَّةً».
Kutoka kwa Thabit bin Dhwahaki- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuunga mkono Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chini ya mti, nakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakaye apa juu ya kiapo cha mila isiyokuwa ya uislamu kwa uongo tena kwa makusudi basi atakuwa kama alivyosema, na atakayeua nafsi kwa kitu chochote ataadhibiwa nacho siku ya kiyama, na hakuna uwajibu juu ya mtu ya kuweka nadhiri katika vile asivyovimiliki" Na katika riwaya nyingine: "Na kumlaani muumini ni sawa na kumuuwa". Na katika riwaya: "Na atakayedai madai ya uongo ili ajichumie (mali) kupitia madai hayo hatomzidishia Mwenyezi Mungu -Mtukufu- isipokuwa upungufu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amepokea Thabit bin Dhwahaki Al-Answariy -mmoja kati ya waliomuunga mkono Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- chini ya mti, katika mkataba wa maridhiano siku ya vita vya hudaibia, kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema katika maana ya maneno yake: Atakaye apa juu ya kiapo kilicho nje ya sheria ya uislamu, mfano akasema: Yeye ni Myahudi au mkristo, au yeye ni majusi, au yeye ni kafiri au kajitenga mbali na Mwenyezi Mungu na Mtume wake itakapokuwa kadhaa wa kadhaa, akadhamiria kusema uongo katika kiapo chake basi atakuwa kama alivyojinasibishia katika moja miongoni mwa mila za kikafiri. Na atakayeiuwa nafsi yake kwa kitu chochote, kama panga, au kisu, au risasi, au kinginecho katika vifaa vya kuulia, ataadhibiwa nacho siku ya kiyama. Na atakayetia nadhiri ya kitu ambacho hakimiliki kama akiweka nadhiri ya kumuacha huru mtumwa wa fulani, au kutoa sadaka katika mali ya fulani, basi nadhiri yake imeharibika na wala haizingatiwi; kwasababu haijaangukia mahala pake, na haijashuka mahala pake. Na atakayemlaani muumini, atakuwa ni kama kamuuwa, kwa kushirikiana mtoa laana na muuwaji kuvunja maharamisho ya Mwenyezi Mungu- Mtukufu- na kuchuma madhambi, na kustahiki adhabu. Na atakayekua na kiburi na akataka wingi wa mali kwa kuleta madai ya uongo yasiyokuwepo, katika mali au elimu au nasaba au utukufu au cheo au kinginecho, akitaka kwa hilo kuongezeka, hatomzidishia Mwenyezi Mungu isipokuwa udhalili na unyonge; kwasababu yeye ametaka kuinyanyua nafsi yake kwa yasiyokuwepo, hivyo malipo yake yataendana na namna ya makusudio yake.
Marejeo
1- صحيح البخاري، دار طوق النجاة ط 1422هـ.
2- صحيح مسلم، ط دار إحياء التراث العربي، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي.
3- الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري.ط دار الفكر، بدمشق، الطبعة الأولى 1381هـ.
4- تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام، تحقيق: محمد صبحي بن حسن حلاق، نشر: الناشر: مكتبة الصحابة، الأمارات - مكتبة التابعين، القاهرة، الطبعة: العاشرة، 1426 هـ - 2006 م.
5- تأسيس الأحكام للنجمي، ط دار المنهاج، 1427هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رَضيَ اللهُ عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «كَفَّارَةُ النَّذْرِ كَفَّارَةُ اليَمِينِ».
Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kafara ya kiapo cha jumla kisipoambatanishwa na kile anachokitaka au kukitaja: Ni kama kafara ya kiapo.
Mafunzo
- Nadhiri: Kisheria: Ni mtu anayelazimika kubeba sheria kujilazimisha yeye mwenyewe kwa hiari yake jambo fulani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kafara ya kiapo: Ni kulisha masikini kumi au kuwavisha kama nguo, au kumuacha huru mtumwa kutoka katika utumwa, asipoweza basi ni kufunga siku tatu.
- Hekima na sababu ya kuwekwa kafara ni Muislamu aiheshimu nadhiri, hivyo asiizoee, na isikae ulimini mwake.
- Aina za nadhiri: 1- Nadhiri isiyoanishwa: Kama mtu kusema: "Nimetia nadhiri ikiwa nitapona" na akanyamaza akawa hakunuia nadhiri maalumu huyu atatakiwa kutoa kafara ya kiapo endapo atapona. 2- Nadhiri ya hamaki na ghadhabu: Nayo ni mtu kutundika nadhiri katika sharti, akiwa na lengo la kukataza jambo kutofanyika au kuwa msukumo wa jambo lifanyike, kama kusema: "Ikiwa nitakusemesha basi nifunge mwezi mzima", na hukumu yake: Apewe hiari kati kufanya alichojiwekea, au atoe kafara ya kiapo wakati atakapomsemesha. 3- Nadhiri ya halali: Mfano: "Natoa nadhiri kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitavaa nguo yangu", na hukumu yake: Atapewa hiari kati ya kuvaa nguo au kutoa kafara ya kiapo. 4- Nadhiri ya machukizo: "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kumpa talaka mke wangu", na hukumu yake: Ni sunna kwake kutoa kafara ya kiapo na asifanye alichotia nadhiri, na akikifanya hatolazimika kutoa kafara. 5- Nadhiri ya maasi: Mfano "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ntakuja kuiba", na hukumu yake ni haramu kuitekeleza, na atatoa kafara ya kiapo, na akitekeleza atapata dhambi lakini hatolazimika kutoa kafara. 6- Nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu: Mfano: "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kuswali rakaa kadhaa" anakusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiitundika katika sharti kama kupona kwa mgonjwa basi ni wajibu kutekeleza endapo sharti litapatikana, na asipoiambatanisha na chochote basi itakuwa wajibu kuitekeleza moja kwa moja.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1265) (1645).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 128).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 135).
منحة العلام شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (5/ 98).
سبل السلام، لمحمد الصنعاني (2/ 558).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com