Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kutoa Bure na Utoaji wa badala.

Hadithi 2

Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama

عَنْ أَبِي حُمَيْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: اسْتَعْمَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا عَلَى صَدَقَاتِ بَنِي سُلَيْمٍ، يُدْعَى ابْنَ اللُّتْبِيَّةِ، فَلَمَّا جَاءَ حَاسَبَهُ، قَالَ: هَذَا مَالُكُمْ وَهَذَا هَدِيَّةٌ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَهَلَّا جَلَسْتَ فِي بَيْتِ أَبِيكَ وَأُمِّكَ، حَتَّى تَأْتِيَكَ هَدِيَّتُكَ إِنْ كُنْتَ صَادِقًا» ثُمَّ خَطَبَنَا، فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَمَّا بَعْدُ، فَإِنِّي أَسْتَعْمِلُ الرَّجُلَ مِنْكُمْ عَلَى العَمَلِ مِمَّا وَلَّانِي اللَّهُ، فَيَأْتِي فَيَقُولُ: هَذَا مَالُكُمْ وَهَذَا هَدِيَّةٌ أُهْدِيَتْ لِي، أَفَلاَ جَلَسَ فِي بَيْتِ أَبِيهِ وَأُمِّهِ حَتَّى تَأْتِيَهُ هَدِيَّتُهُ، وَاللَّهِ لاَ يَأْخُذُ أَحَدٌ مِنْكُمْ شَيْئًا بِغَيْرِ حَقِّهِ إِلَّا لَقِيَ اللَّهَ يَحْمِلُهُ يَوْمَ القِيَامَةِ، فَلَأَعْرِفَنَّ أَحَدًا مِنْكُمْ لَقِيَ اللَّهَ يَحْمِلُ بَعِيرًا لَهُ رُغَاءٌ، أَوْ بَقَرَةً لَهَا خُوَارٌ، أَوْ شَاةً تَيْعَرُ» ثُمَّ رَفَعَ يَدَهُ حَتَّى رُئِيَ بَيَاضُ إِبْطِهِ، يَقُولُ: «اللَّهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ» بَصْرَ عَيْنِي وَسَمْعَ أُذُنِي.
Kutoka kwa Abuu Humaid Assaaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja akiitwa: Bin Lutbia ya kukusanya Zaka kutoka katika kabila la Bani Suleim, aliporejea Madina akampa mahesabu ya mali aliyokusanya na aliyotumia, akasema bin Lutbia: Hii ndio mali yenu niliyoikusanya kutoka katika Zaka, na mali hii nimepewa zawadi mimi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake kumwambia: Hivi si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako ili uone je utapewa zawadi ikiwa wewe ni mkweli; kwani hakika haki ulizozifanyia kazi ndio sababu ya kupewa kwako zawadi, na kwamba lau ungekaa nyumbani kwako usingezawadiwa chochote, hupaswi kuihalalisha kwakuwa tu imekufikia kwa njia ya zawadi. Kisha akapanda Mimbari rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya kuhutubia huku akiwa na hasira, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni kama mfanya kazi na muajiriwa katika kile ambacho Mwenyezi Mungu kanipa maamuzi ndani yake miongoni mwa Zaka na Ngawira, kisha anakuja kutoka katika kazi yake na anasema: Hii ni yenu na hii ni zawadi yangu nimezawadiwa! Kwa nini asikae nyumbani kwa baba yake na mama yake ili zawadi yake imfuate, Wallah, namuapa Mwenyezi Mungu, hatochukua yeyote chochote katika vile anavyopewa isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kakibeba siku ya Kiyama juu ya shingo yake, ikiwa alichokichukua ni Ngamia mwenye sauti, au Ng'ombe mwenye sauti ya mroromo, au mbuzi mwenye mlio, basi atapiga kelele. Kisha akanyanyua mikono yake kwa kasi mpaka waliokaa wakaona weupe wa kwapa lake, kisha akasema: Shuhudieni kuwa nimefikisha hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenu. Kisha Abuu Humaidi Assaaidi akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Kuwa haya ni miongoni mwa mambo ambayo macho yake yaliyashuhudia na masikio yake yakayasikia.

Mafunzo
  1. Inatakiwa kwa Hakimu kuwabainishia anaofanya nao kazi wajibu wao na yasiyotakiwa katika kazi zao.
  2. Ahadi kali kwa anayechukua mali za watu kwa dhulma.
  3. Hakuna atakayedhulumu isipokuwa atakuja na kila alichodhulumu siku ya Kiyama.
  4. La wajibu kwa muajiriwa katika kazi yoyote miongoni mwa kazi za nchi atimize majukumu aliyopewa, na hatakiwi kuchukua zawadi katika kile kinachohusiana na kazi yake, na akichukua basi akiweke katika benki ya Waislamu, na haifai kuichukua kwa matumizi yake binafsi, kwa sababu hilo ni njia ya kwenda katika shari na kupoteza amana.
  5. Amesema bin Battwal: Hadithi imeonyesha kuwa zawadi kwa mfanya kazi inakuwa ni shukurani kwa wema wake, au kwa ajili ya kujipendekeza kwake, au kumtaka asitende haki, akaashiria Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa anachozawadiwa yeye katika hivyo yuko sawa na Waislamu wengine, hana ubora kuliko wao katika hicho, na kwamba haifai kujipendelea.
  6. Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Kumebainishwa kuwa zawadi zote za wafanya kazi ni haramu na ni wizi; kwa sababu atakuwa kafanya hiana katika uongozi wake na amana yake, na ndio maana akataja katika hadithi katika adhabu yake na kumbebesha kwake kile alichozawadiwa siku ya Kiyama, kama alivyotaja mfano kwa mwenye kuficha mali, na amebainisha rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii sababu ya kuharamisha zawadi, ambayo ni uongozi, kinyume na zawadi ya mtu ambaye si mfanya kazi, kwani hiyo inafaa kuchukua.
  7. Amesema bin Munir: Inachukuliwa katika kauli yake: "kwa nini asingekaa nyumbani kwa baba yake na mama yake" Kuwa inafaa kupokea zawadi kutoka kwa yule aliyekuwa akimpa zawadi kabla ya hapo, amesema bin Hajar: Na haifichikani kuwa mahali pake nikuwa isizidi kiwango cha kawaida.
  8. Mfumo wa Mtume katika utoaji wa nasaha, ni kuzungumza kwa watu wote, na si kumtangaza mtu.
  9. Amesema bin Hajari: Hapa inaonyesha kuwa ni sheria kumkagua aliyepewa dhamana.
  10. Amesema bin Hajari: Na inaonyesha kuwa inafaa kumkemea aliyekosea.
  11. Inapendeza kunyanyua mikono katika dua.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 28) (6979). صحيح مسلم (3/ 1463) (1832). جمهرة اللغة، أبوبكر الأزدي (2/ 1067). المعجم الوسيط، مجمع اللغة العربية (2/ 1065). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 305). تطرز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص166). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 234).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Peaneni zawadi, mtapendana

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «تَهَادَوا تَحَابُّوا».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- anasema: "Peaneni zawadi, mtapendana."
Imepokelewa na Bukhari katika Al-Adab Al-Mufrad na Abuu Ya'laa na Al-BayhaqiyDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza Muislamu kuwa abadilishane zawadi na ndugu yake Muislamu, na kuwa zawadi ni miongoni mwa sababu za mapenzi na kuziunganisha nyoyo.

Mafunzo
  1. Ni sunna kutoa zawadi; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha kufanya hivyo.
  2. Zawadi ni sababu ya kuleta mapenzi.
  3. Inampasa mwanadamu afanye kila ambacho ndani yake kinaleta mapenzi kati yake na watu wengine, sawa sawa iwe ni katika zawadi au kuwa mpole, au katika maneno mazuri au katika ukunjufu wa uso kwa kadiri awezavyo.
Marejeo

الأدب المفرد للبخاري (ص:208) (594). مسند أبي يعلى الموصلي (11/ 9) (6148). السنن الكبرى للبيهقي (6/ 169). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام (4/ 319). فيض القدير (3/ 271). التيسير بشرح الجامع الصغير (1/ 457).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com