عَنْ أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا مِنْ صَاحِبِ ذَهَبٍ وَلَا فِضَّةٍ، لَا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا، إِلَّا إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ، صُفِّحَتْ لَهُ صَفَائِحُ مِنْ نَارٍ، فَأُحْمِيَ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ، فَيُكْوَى بِهَا جَنْبُهُ وَجَبِينُهُ وَظَهْرُهُ، كُلَّمَا بَرَدَتْ أُعِيدَتْ لَهُ، فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، حَتَّى يُقْضَى بَيْنَ الْعِبَادِ، فَيَرَى سَبِيلَهُ، إِمَّا إِلَى الْجَنَّةِ، وَإِمَّا إِلَى النَّارِ»
قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، فَالْإِبِلُ؟ قَالَ: «وَلَا صَاحِبُ إِبِلٍ لَا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا، وَمِنْ حَقِّهَا حَلَبُهَا يَوْمَ وِرْدِهَا، إِلَّا إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ، بُطِحَ لَهَا بِقَاعٍ قَرْقَرٍ، أَوْفَرَ مَا كَانَتْ، لَا يَفْقِدُ مِنْهَا فَصِيلًا وَاحِدًا، تَطَؤُهُ بِأَخْفَافِهَا وَتَعَضُّهُ بِأَفْوَاهِهَا، كُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ أُولَاهَا رُدَّ عَلَيْهِ أُخْرَاهَا، فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، حَتَّى يُقْضَى بَيْنَ الْعِبَادِ، فَيَرَى سَبِيلَهُ إِمَّا إِلَى الْجَنَّةِ، وَإِمَّا إِلَى النَّارِ»
قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، فَالْبَقَرُ وَالْغَنَمُ؟ قَالَ: «وَلَا صَاحِبُ بَقَرٍ، وَلَا غَنَمٍ، لَا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا، إِلَّا إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ بُطِحَ لَهَا بِقَاعٍ قَرْقَرٍ، لَا يَفْقِدُ مِنْهَا شَيْئًا، لَيْسَ فِيهَا عَقْصَاءُ، وَلَا جَلْحَاءُ، وَلَا عَضْبَاءُ تَنْطَحُهُ بِقُرُونِهَا وَتَطَؤُهُ بِأَظْلَافِهَا، كُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ أُولَاهَا رُدَّ عَلَيْهِ أُخْرَاهَا، فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، حَتَّى يُقْضَى بَيْنَ الْعِبَادِ، فَيَرَى سَبِيلَهُ إِمَّا إِلَى الْجَنَّةِ، وَإِمَّا إِلَى النَّارِ»
قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، فَالْخَيْلُ؟ قَالَ: «الْخَيْلُ ثَلَاثَةٌ: هِيَ لِرَجُلٍ وِزْرٌ، وَهِيَ لِرَجُلٍ سِتْرٌ، وَهِيَ لِرَجُلٍ أَجْرٌ، فَأَمَّا الَّتِي هِيَ لَهُ وِزْرٌ، فَرَجُلٌ رَبَطَهَا رِيَاءً وَفَخْرًا وَنِوَاءً عَلَى أَهْلِ الْإِسْلَامِ، فَهِيَ لَهُ وِزْرٌ، وَأَمَّا الَّتِي هِيَ لَهُ سِتْرٌ، فَرَجُلٌ رَبَطَهَا فِي سَبِيلِ اللهِ، ثُمَّ لَمْ يَنْسَ حَقَّ اللهِ فِي ظُهُورِهَا وَلَا رِقَابِهَا، فَهِيَ لَهُ سِتْرٌ وَأَمَّا الَّتِي هِيَ لَهُ أَجْرٌ، فَرَجُلٌ رَبَطَهَا فِي سَبِيلِ اللهِ لِأَهْلِ الْإِسْلَامِ، فِي مَرْجٍ وَرَوْضَةٍ، فَمَا أَكَلَتْ مِنْ ذَلِكَ الْمَرْجِ، أَوِ الرَّوْضَةِ مِنْ شَيْءٍ، إِلَّا كُتِبَ لَهُ، عَدَدَ مَا أَكَلَتْ حَسَنَاتٌ، وَكُتِبَ لَهُ، عَدَدَ أَرْوَاثِهَا وَأَبْوَالِهَا، حَسَنَاتٌ، وَلَا تَقْطَعُ طِوَلَهَا فَاسْتَنَّتْ شَرَفًا، أَوْ شَرَفَيْنِ، إِلَّا كَتَبَ اللهُ لَهُ عَدَدَ آثَارِهَا وَأَرْوَاثِهَا حَسَنَاتٍ، وَلَا مَرَّ بِهَا صَاحِبُهَا عَلَى نَهْرٍ، فَشَرِبَتْ مِنْهُ وَلَا يُرِيدُ أَنْ يَسْقِيَهَا، إِلَّا كَتَبَ اللهُ لَهُ، عَدَدَ مَا شَرِبَتْ، حَسَنَاتٍ»
قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، فَالْحُمُرُ؟ قَالَ: «مَا أُنْزِلَ عَلَيَّ فِي الْحُمُرِ شَيْءٌ، إِلَّا هَذِهِ الْآيَةَ الْفَاذَّةُ الْجَامِعَةُ»: {فَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ، وَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ} [الزلزلة: 8].
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni, basi litachemshwa katika moto wa Jahanam, kisha zitapigwa pasi mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila linapopoa linarejeshewa umoto, katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, (atadumu katika adhabu hiyo) mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake, ima inakwenda peponi, na ima anakwenda motoni" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi kuhusu Ngamia? Akasema: "Wala mmiliki wa Ngamia asiyetekeleza haki yake, na miongoni mwa haki zake ni kuwakamua siku wanapotoka manyweshoni, isipokuwa (asipofanya hivyo) itakapofika siku ya Kiyama atalazwa kifudifudi katika eneo tambarare lenye kina kirefu kisha wataletwa wanyama wake kwa wingi zaidi ya jinsi walivyokuwa duniani, hatokosekana hata ndama mmoja, kisha wataanza kumkanyaga kwa kwato zao, na watakuwa wakimng'ata kwa midomo yao, kila anapopita wa mwanzo wao anarejeshwa mpaka wa mwisho wao, na (adhabu hii ataendelea nayo) katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake ima anakwenda peponi au anakwenda motoni" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Vipi kuhusu Ng'ombe na Mbuzi? Akasema: "Wala mmiliki wa Ng'ombe na Mbuzi, asiyetekeleza haki zake, isipokuwa itakapofika siku ya Kiyama atalazwa chini katika Ardhi tambarare yenye kina, hakuna mnyama yeyote atakayekosekana, na hakuna aliyepinda pembe wala aliyejeruhiwa, wala aliyekatika pembe watakuwa wakimchoma kwa pembe zao na wakimkanyaga kwa kwato zao, kila akimpitia wa mwanzo wake, anarejeshwa wa mwisho wao, atabaki hivyo mpaka watakapohukumiwa waja, na hapo ataona njia yake, ima anakwenda peponi, na ima anakwenda motoni". Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi kuhusu Farasi? Akasema: "Farasi wana aina tatu: Wapo ambao ni mzigo kwa mtu, na wapo wanaomsitiri mtu, na wapo wanaomuingizia malipo mtu, ama ambao ni mzigo kwa mtu ni mtu aliyewafunga kwa kujionyesha na kutaka ufahari kwa watu, na ama kuhusu wale ambao ni stara kwake ni wale ambao mtu amewafunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi hakusahau haki ya Mwenyezi Mungu katika migongo yao wala shingo zao, Farasi hao kwake ni kinga na ni stara, ama ambao kwake ni malipo, ni mtu aliyewafunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya waislamu, katika malisho na viuga, isipokuwa ataandikiwa malipo ambayo idadi yake itakwenda sawa na idadi watakayokula Farasi hao, na wala hayatokatwa manyoa yake kisha yakastawi vizuri au vizuri zaidi isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi ya athari zake na kinyesi chake, na wala mmiliki huyo hatowapitisha mtoni wakanywa katika mto huo, hata kama hakukusudia kuwapeleka manyweshoni, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi watakayokunywa hapo"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amebainisha makundi ya mali, na malipo ya mtu ambaye hatotekeleza zaka yake siku ya Kiyama, na miongoni mwake:
Ya kwanza: Dhahabu na fedha na vyote vilivyo katika hukumu ya hivyo miongoni mwa mali na bidhaa za biashara, nazo ni zile za wajibu ndani yake kutolewa zaka ikawa hazikutekelezwa, itakapofika siku ya Kiyama zitayeyushwa na kumiminwa na kutengenezwa katika umbile la sahani, na zitawashwa na kuchemshwa katika moto wa Jahannam, na ataadhibiwa nazo mwenye nazo, zitapigwa pasi kwazo mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila ikipoa inachemshwa tena, na ataendelea katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambao makadirio ya siku yake ni siku elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohumu kati ya viumbe, hapo ima awe ni katika watu wa peponi au watu wa motoni.
Wa pili: Ni mmiliki wa ngamia ambaye hatekelezi faradhi ya zaka zake na haki zake, ikiwemo kuwakamua na kumpatia maziwa anayehudhuria wakati wa kukamua miongoni mwa masikini, wataletwa ngamia hawa wakiwa wakubwa tena walionenepa, na wakiwa wengi kwa idadi zaidi ya jinsi walivyokuwa, na mmiliki wake atatupwa na kulazwa chini na kunyooshwa vizuri siku ya Kiyama katika Ardhi pana ya tambarare, watakuwa wakimkanyaga kwa miguu yao na wakimng'ata kwa meno yao, kila akipita wa mwisho wao, anarejeshwa wa mwanzo wao, na ataendelea katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambayo kiasi chake ni siku elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina ya viumbe, na hapo atakuwa ni miongoni mwa watu wa peponi au watu wa motoni.
Wa tatu: Ni mmiliki wa ng'ombe na mbuzi -ikiwemo kondoo- ambazo mmiliki wake hatekelezi zaka yake ya faradhi, zitaletwa zikiwa kamili kwa wingi zaidi ya jinsi zilivyokuwa, hakuna mnyama atakayepungua, atanyooshwa vizuri na kutupwa na atalazwa huyo mmiliki wake siku ya Kiyama katika Ardhi pana ya tambarare, hakuna mnyama atakayekuwa na pembe zilizopinda, wala asiyekuwa na pembe, wala aliyevunjika pembe, bali watakuwa katika maumbile yao kamili, watakuwa wakimchoma kwa pembe zao, na wakimkanyaga kwa miguu yao, kila akipita wa mwisho wao anarejeshwa wa mwanzo wao, Na ataendelea kuwa katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambayo kiasi chake ni miaka elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina ya viumbe, na hapo atakuwa miongoni mwa watu wa peponi au watu wa motoni
Ya nne: Mfugaji wa Farasi, naye ana aina tatu:
Aina ya kwanza: Ni farasi ambao ni mzigo, nao ni wale ambao mtu kawafuga kwa lengo la kutaka kuonekana kwa watu, na kujifaharisha na kwa lengo la kuwapiga vita waislamu.
Aina ya pili: Ambao kwake ni stara, nao ni wale ambao mtu kawaandaa kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha akawapa matunzo, akasimamia malisho yake na mahitaji yake mengine, ikiwemo kuyaachia madume haki yake.
Aina ya tatu: Ambao kwake ni malipo, nao ni wale ambao mtu kawafuga kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waislamu, akawaweka katika uwanja wa malisho kwa ajili ya chakula, hakuna watakachokula hapo isipokuwa ataandikiwa mema kwa idadi ya kile walichokula, na ataandikiwa mema kwa kila kinyesi chao na mikojo yao, na wala hawatokata kamba yao wanayofungwa nayo, wakakimbia na kutimka mbio katika maeneo yenye miinuko katika Ardhi, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa kila athari (alama) ya unyayo na kinyesi chao, na wala mmiliki wake hatowapitisha katika mto wakanywa katika mto huo, hata kama hakukusudia kuwanywesha isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi ya fundo walizokunywa.
Kisha akaulizwa rehema na amani ziwe juu yake kuhusu punda wa mjini je naye mtu atampatia malipo mfano wa farasi?
Akasema kuwa: Haijateremshwa sheria yoyote kuhusu hilo isipokuwa aya hizi chache kimtazamo, ambazo zinakusanya kila aina ya ibada na maasi; nayo ni kauli yake Mtukufu: "Basi yeyote atakayefanya uzito wa chembe ndogo jema basi ataliona, na yeyote atakayefanya uzani wa chembe ndogo jambo baya basi ataliona". [Azzalza: 8], atakayefanya jambo jema katika ufugaji wa punda basi naye thawabu za hilo ataziona, na endapo atafanya maasi basi ataiona adhabu yake, na hii inajumuisha amali zote.
Mafunzo
- Uwajibu wa kutoa zaka, na ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kuzuia.
- Hakufuru mtu aliyezuia kutoa zaka kwa uzembe, lakini yupo katika hatari kubwa.
- Mwanadamu hulipwa kwa kila kipengele kinachotokea katika ibada, endapo atakusudia kupata malipo toka mwanzo wa kitu, hata kama hatokusudia mchanganuo huo.
- Katika mali kuna haki zingine nje ya zaka.
- Miongoni mwa haki katika ngamia ni kumkamulia maziwa anayehudhuria wakati wa manywesho yao katika masikini; ili kumrahisishia muhitaji kupata nguvu ya kufika nyumbani, na nikuwapunguzia mzigo wanyama, anasema bin Battwal: Katika mali kuna haki mbili: Faradhi ya lazima, na faradhi ya kujitosheleza, kuwakamulia watu maziwa ni katika haki ambazo huhesabika ni katika tabia njema.
- Miongoni mwa haki za wajibu katika ngamia na ng'ombe ni kuliachia dume endapo litahitaji kupanda.
- Hukumu ya punda na vyote ambavyo havikutajwa katika sheria nikuwa: Vyote vinaingia ndani ya kauli yake Mtukufu: "Yeyote atakayefanya uzito wa chembe ndogo jambo jema basi ataliona, na atakayefanya uzito wa chembe ndogo ya jambo baya basi ataliona".
- Aya inahamasisha katika kufanya heri japo ndogo, na inahofisha kufanya shari hata ikiwa yakudharauliwa.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 175) (4962).
صحيح مسلم (2/ 680) (987).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين.
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 350).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 862).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 253).
تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان، لعبد الرحمن آل سعدي (ص335).
فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر (3/ 268).
شرح الزرقاني على موطأ مالك، لمحمد الزرقاني (2/ 164).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1262).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «إِذَا مَاتَ الْإِنْسَانُ انْقَطَعَ عَنْهُ عَمَلُهُ إِلَّا مِنْ ثَلَاثَةٍ: إِلَّا مِنْ صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ، أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amali za maiti hukatika kwa kufa kwake, hayapatikani mema tena baada ya kifo chake isipokuwa kwa mambo haya matatu; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya kupatikana kwake:
La kwanza: Sadaka yenye kuendelea thawabu zake na kudumu, isiyokatika, kama wakfu, na kujenga msikiti, na kuchimba visima, na mengineyo.
La pili: Elimu wanayonufaika nayo watu, kama kutunga vitabu vya kielimu, au kama kumfundisha mtu, yule naye akaisambaza elimu hiyo baada ya kifo chake.
La tatu: Mtoto mwema muumini wa kumuombea dua mzazi wake.
Mafunzo
- Wamekubaliana wanachuoni kuwa katika mambo yanayomfuata mwanadam baada ya kufa kwake katika thawabu ni: Sadaka ya kuendelea, na elimu yenye kunufaisha watu, na dua, na imekuja Hija katika hadithi zingine pia.
- Yametajwa mambo haya matatu pekee katika hadithi; kwa sababu ndio msingi wa mambo ya kheri, na ndio mambo wanayoyafanya watu wema wengi baada ya kuondoka kwao.
- Kila elimu yenye kunufaisha basi hupatikana malipo kwa elimu hiyo, lakini kilele chake ni elimu ya kisheria na elimu za msingi kwake.
- Elimu ndiyo yenye manufaa zaidi kati ya haya matatu; Kwa sababu elimu inamnufaisha mtu anayeisoma, elimu inahusisha kuihifadhi Sheria, inawanufaisha watu kwa ujumla, na ni pana zaidi na ni ya jumla, kwa sababu anajifunza kutoka katika elimu yako aliyepo wakati wa uhai wako na atakayekuwepo baada ya kufa kwako.
- Himizo la kulea watoto wema; Wao ndio wanaowanufaisha wazazi wao Akhera, na miongoni mwa manufaa yao ni kuwaombea dua.
- Himizo la kuwatendea wema wazazi wawili baada ya kufa kwako, nao ni katika wema ambao mtoto anafaidika nao.
- Dua inamnufaisha maiti hata kama haikutoka kwa mtoto, lakini katajwa mtoto pekee kwa sababu ndiye atakayeendelea kumuombea dua mtu mara nyingi mpaka kufa kwake.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1255) (1631)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (28/ 413).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن سعد بن عبادة رضي الله عنه أنه قال: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أُمَّ سَعْدٍ مَاتَتْ، فَأَيُّ الصَّدَقَةِ أَفْضَلُ؟، قَالَ: «الْمَاءُ»، قَالَ: فَحَفَرَ بِئْرًا، وَقَالَ: هَذِهِ لِأُمِّ سَعْدٍ.
Kutoka kwa Sa'di bin Ubada radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di.
Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn MajahDarajaHassani kwa mkusanyiko wa njia zake
Maelezo
Alifariki mama Sa'di bin Ubada radhi za Allah ziwe juu yake, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni aina ipi bora ya sadaka ili aitoe kwa niaba ya mama yake? Akamueleza rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa sadaka bora ni maji, akachimba kisima na akakifanya kuwa sadaka kwa ajili ya mama yake.
Mafunzo
- Kumeelezwa kuwa maji ndio sadaka bora zaidi.
- Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Sa'di katika sadaka ya maji; kwa sababu ndio inamanufaa mapana katika mambo ya dini na dunia, na kwa sababu ya joto kali na haja ya watu na uchache wa maji.
- Hii ni dalili kuwa malipo ya sadaka yanawafikia maiti.
- Wema wa Sa'di bin Ubada kwa mama yake radhi za Allah ziwe juu yao.
Marejeo
سنن أبي داود (3/ 109) (1681)، سنن النسائي (6/ 254) (3664)، سنن ابن ماجه (4/ 643) (3684)، شرح سنن أبي داود للعباد (204/ 19).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com