Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الذَّهَبُ بِالذَّهَبِ، وَالْفِضَّةُ بِالْفِضَّةِ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ، وَالْمِلْحُ بِالْمِلْحِ، مِثْلًا بِمِثْلٍ، سَوَاءً بِسَوَاءٍ، يَدًا بِيَدٍ، فَإِذَا اخْتَلَفَتْ هَذِهِ الْأَصْنَافُ، فَبِيعُوا كَيْفَ شِئْتُمْ، إِذَا كَانَ يَدًا بِيَدٍ».
Kutoka kwa Ubada bin Swaamit -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake namna ya biashara sahihi katika aina sita za riba, nazo ni: Dhahabu, fedha, ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano (iliyokobolewa), na tende, na chumvi, ikiwa ni katika aina hiyo hiyo, kama kuuza dhahabu kwa dhahabu na fedha kwa fedha....ni lazima kuwe na sharti mbili: Ya kwanza: Kufanana katika uzito ikiwa ni kitu kinachopimika kama dhahabu na fedha, au kufanana katika kipimo ikiwa ni kitu kinachopimika, kama ngano (ambayo haijakobolewa) na ngano (iliyokobolewa) na tende na chumvi. Ya pili: Ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa, na hilo lifanyike katika kikao cha makubaliano ya biashara. Zikitofautiana aina zote hizi kama kuuza dhahabu kwa fedha, na tende kwa ngano kwa mfano, itafaa kuuza kwa sharti moja, nayo ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa katika kikao cha makubaliano, isipofanyika hivyo biashara itakuwa batili, na muuzaji na mnunuzi watakuwa wameingia ndani ya riba katika hilo wote wawili.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa mali zinahusika katika riba na namna ya kuuza ndani yake.
  2. Katazo la kuuza kwa riba.
  3. Fedha za noti au sarafu zinachukua hukumu ya dhahabu na fedha katika sababu ya riba yake.
  4. Kuuza na kununua aina hizi sita zenye kuhusika katika riba kuna hali nyingi: 1- Ni kuuzwa riba kwa riba kwa aina hiyo hiyo, kama dhahabu kwa dhahabu na tende kwa tende.... na ni sharti kusihi kwake kuwe na sharti mbili: 1- Kufanana katika uzani au kilo, na kukabidhiana katika kikao cha makubaliano, 2- Ni kuuzwa riba kwa riba kwa aina tofauti ikiwa ni pamoja na kufanana kwa sababu, kama dhahabu kwa fedha, na ngano isiyokobolewa kwa ngano iliyokobolewa, ni sharti kuwe na kukabidhiana, pasina kufanana, 3- Ni kuuza riba kwa riba kwa aina tofauti ikiwa ni pamoja na kutofautiana sababu, katika hilo hakuna sharti la kukabidhiana, wala mfanano kama kuuza dhahabu kwa tende.
  5. Kuuza na kununua aina zisizokuwa na uhusiano na riba, au moja wake ikawa ni ya riba na nyingine si riba; na ni sharti katika hilo kukabidhiwa, na wala hakuna sharti la kufanana, kama kuuza jengo kwa dhahabu.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1210) (1587). فيض القدير (3/ 571). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (27/ 623).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Riba.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com