عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ، شِبْرًا بِشِبْرٍ، وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ، حَتَّى لَوْ دَخَلُوا فِي جُحْرِ ضَبٍّ لَاتَّبَعْتُمُوهُمْ» قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ آلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى؟ قَالَ: «فَمَنْ؟».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: “Hakika mtafuata njia za walio kuwa kabla yenu, hatua kwa hatua, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia kwenye pango la mburukenge, mtawafuata.” Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unakusudia Mayahudi na Wakristo? Akasema: “Kwa hiyo ni nani?”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, jinsi hali ya baadhi ya watu wa Umma wake watakavyokuwa baada ya zama zake, ambako ni kufuata njia ya Mayahudi na Wakristo katika imani, matendo, desturi na mila zao, kufuata kwa undani sana, inchi kwa inchi, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia katika tundu la mburukenge, nao wataingia nyuma yao.
Mafunzo
- Hii ni alama miongoni mwa alama za utume wake, kwani alilieleza hilo kabla halijatokea, na limetokea kama alivyoeleza.
- Katazo la Waislamu kuwaiga makafiri, iwe katika imani zao, ibada, sherehe, au nguo zao maalum kwa ajili yao.
- Kufafanua mambo ya yasiyoonekana kwa mifano ya vitu vyenye kuonekana, hii ni katika mbinu za kufundishia katika Uislamu.
- Mburukenge: Ni mnyama ambaye shimo lake lina giza kupindukia na lina harufu mabaya. Ni mtambaazi ambaye hupatikana kwa wingi jangwani, na sababu ya kufananisha na shimo la mburukenge ni wembamba wake sana na ubaya wake. Hata hivyo, kwa sababu ya kufuata mienendo yao, na kufuata kwao njia zao, laiti wangeingia kwenye wembamba huu mbaya namna hiyo, basi wangelikubaliana nao! Tunamuomba Mwenyezi Mungu Msaada!.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 103) (7320).
صحيح مسلم (4/ 2054) (2669).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص213).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص193).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم: «مَن تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ».
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye jifananisha na watu fulani katika makafiri au waovu au wema -na hii ni pale atakapofanya jambo katika mambo yao mahususi, kama itikadi au ibada au tamaduni basi naye ni miongoni mwao-; kwa sababu kujifananisha nao katika muonekano kunapelekea kujifananisha nao kiundani, na hakuna shaka kuwa kujifananisha na watu fulani kunasababishwa na kupendezwa nao, na huenda kukapelekea kuwapenda na kuwatukuza na kuwategemea, na hili huenda likampelekea mtu hata kujifananisha kiundani na katika ibada -Tunamuomba Allah atukinge na hilo-.
Mafunzo
- Tahadhari ya kujifananisha na makafiri na waovu.
- Himizo la kujifananisha na watu wema na kuiga kutoka kwao.
- Kujifananisha katika muonekano hutia mapenzi katika moyo.
- Mtu hupata kemeo la adhabu na madhambi kulingana na namna ya kujifananisha na aina yake.
- Katazo la kujifananisha na makafiri katika dini yao na katika desturi zao mahususi kwao, ama yasiyokuwa hayo kama kujifunza ufundi na mfano wake hayaingii katika katazo.
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 144) (4031).
مسند أحمد (9/ 126) (5115).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 363).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 157).
فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 335).
مشكاة المصابيح، للتبريزي (2/ 1246).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم الرجل يلبس لِبْسَةَ المرأة، والمرأة تلبس لِبْسَةَ الرجل.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.
Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah kwa maana yake na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu kwa kila mwanaume atakayejifananisha na mwanamke katika mavazi maalumu kwa ajili ya wanawake; sawa sawa iwe katika muonekano au rangi au jinsi au namna ya uvaaji na kujipamba. Au kwa mwanamke kujifananisha na mavazi maalumu kwa wanaume vile vile, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.
Mafunzo
- Amesema Shaukani: Kumeharamishwa wanawake kujifananisha na wanaume na wanaume kujifananisha na wanawake; kwa sababu laana huwa haiwi ila kwa kufanya jambo lililoharamishwa.
- Amesema bin Uthaimiin: Zile wanazoshirikiana kati yao, mfano kama jezi au shati ambazo wanazivaa wanaume na wanawake hizi hazina tatizo, yaani hakuna tatizo akizivaa mwanaume na mwanamke; kwa sababu wanashirikiana.
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 195) (4098).
السنن الكبرى للنسائي (8/ 297) (9209).
سنن ابن ماجه (3/ 95) (1903).
مسند أحمد (14/ 61) (8309).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1122).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (19/ 337).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 150).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 370).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com