Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu za Kupenda na Kuchukia.

Hadithi 3

Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake

عن أبي هريرة رضي الله عنه أَن النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: «الرَّجُلُ عَلَى دِينِ خَلِيلِهِ، فَلْيَنْظُر أَحَدُكُم مَنْ يُخَالِل».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu hufanana na rafiki na jamaa yake wa dhati katika nyenendo na tabia zake, na urafiki huathiri maadili, tabia na matendo, na kwa ajili hiyo alielekeza vyema katika uchaguzi wa rafiki. Kwa sababu atamuongoza rafiki yake katika imani na uongofu na kheri, na atakuwa ni msaada kwa rafiki yake.

Mafunzo
  1. Amri ya kusuhubiana na wema na kuwachambua, na katazo la kusuhubiana na watu wabaya.
  2. Ametajwa rafiki badala ya ndugu; Kwa sababu wewe ndiye unayemchagua rafiki, lakini ndugu na jamaa, huna chaguo.
  3. Kumchukua mtu kuwa rafiki lazima kuanze na kutafakari.
  4. Mtu huiimarisha dini yake kwa kusuhubiana na waumini na huidhoofisha kusuhubiana na watu waovu.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 204) (4833). سنن الترمذي (4/ 187) (2378). مسند أحمد (13/ 398) (8028). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 433). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، للمباركفوري (7/ 51). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص250). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 166). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 341).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ سِتٌّ» قِيلَ: مَا هُنَّ يَا رَسُولَ اللهِ؟، قَالَ: «إِذَا لَقِيتَهُ فَسَلِّمْ عَلَيْهِ، وَإِذَا دَعَاكَ فَأَجِبْهُ، وَإِذَا اسْتَنْصَحَكَ فَانْصَحْ لَهُ، وَإِذَا عَطَسَ فَحَمِدَ اللهَ فَسَمِّتْهُ، وَإِذَا مَرِضَ فَعُدْهُ وَإِذَا مَاتَ فَاتَّبِعْهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu ni mambo sita: La kwanza: Amsalimie akikutana naye kwa kusema: Assalaam alaikum, naye atajibu salamu kwa kusema: Waalaikumussalaam. La pili: Kuitika wito wake atakapomuita kwa ajili ya sherehe ya harusi au nyingineyo. La tatu: Kumpa nasaha akizihitajia, na wala usimsifie bure, au kumfanyia udanganyifu. La nne: Akipiga chafya akasema: Alhamdulillaah, basi muombee dua kwa kusema: Yar-hamkallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu), naye ajibu kwa kusema: Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum (Akuongozeni Mwenyezi Mungu na kutengenezeeni hali zenu). La tano: Akamuone na amtembelee atakapougua. La sita: Amswalie atakapofariki, na alisindikize jeneza lake mpaka azikwe.

Mafunzo
  1. Amesema Shaukani: Na makusudio ya kauli yake: (Haki za muislamu) Nikuwa haitakiwi kuziacha, na kunakuwa kuzifanya kwake ima ni wajibu au sunna iliyotiwa mkazo inayofanana na wajibu ambayo haitakikani kuiacha.
  2. Kujibu salamu ni faradhi ya lazima, mwenye kusalimiwa atakapokuwa mmoja, na wakiwa wengi basi mmoja anatosheleza, ama kuanza salamu asili yake ni sunna.
  3. Mgonjwa kutembelewa ni katika haki zake juu ya ndugu zake waislamu; kwa sababu humuingizia furaha na liwazo ndani ya moyo wake, na ni faradhi ya kujitosheleza, wakifanya wenye kutosheleza basi wengine hawana dhambi.
  4. Uwajibu wa kuitika wito kukiwa hakuna madhmbi ndani yake; ikiwa ni wito wa sherehe ya harusi basi jopo la wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kuitika, isipokuwa kukiwa na udhuru wa kisheria, ama ikiwa si sherehe ya harusi jopo la wanachuoni wakasema kuwa ni sunna.
  5. Kumuombea dua aliyepiga chafya ni wajibu juu ya yule aliyesikia kumhimidiwa Mwenyezi Mungu mpiga chafya.
  6. Ukamilifu wa sheria na pupa yake katika kuunganisha nguvu na umoja wa jamii na imani, na nyenzo za mapenzi kati ya mtu mmoja mmoja.
  7. "Muombee rehema" Yaani kumuombea dua ya kheri na baraka, na tashmiiti (kumuombea dua) imesemekana maana yake: Mwenyezi Mungu akuweke mbali na kuchekwa na maadui, na ayaweke mbali nawe yale yatakayofanya adui yako akucheke, na tasmiit (kwa siin): Maana yake: Mwenyezi Mungu akuongoze katika ustaarabu ulionyooka.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1705) (2162). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 7). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (3/ 128). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 327).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu

عن أبي صِرْمة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ ضَارَّ ضَارَّ اللهُ بِهِ، وَمَنْ شَاقَّ شَقَّ اللهُ عَلَيْهِ».
kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutomuingizia madhara muislamu, au kumtia tabu katika jambo lolote katika mambo yake; Yeye mwenyewe au mali yake au familia yake, nakuwa atakayefanya hivyo basi Mwenyezi Mungu atamlipa na atamuadhibu kwa jinsi alivyomfanyia mwenzake.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kumdhuru muislamu na kumtia tabu.
  2. Allah huwalipizia kisasi waja wake.
Marejeo

سنن أبي داود (5/ 477) (3635). سنن الترمذي (3/ 495) (1940). سنن ابن ماجه (3/ 432) (2342). مسند أحمد (25/ 34) (15755). مساوئ الأخلاق، للخرائطي (ص: 274) (583). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، للبسام (7/ 445). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 396). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 261).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com