عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الحَسَن والحُسَيْن سَيِّدا شَباب أهْل الجنة».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa wajukuu zake Hassan na Hussein watoto wa Ally bin Abii Twalib na Fatma binti wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na Allah amridhie, wao ni mabosi katika fadhila wa kila aliyekufa akiwa kijana na akaingia peponi, au wao ni mabosi wa vijana wa watu wa peponi, kasoro Manabii na Mahalifa (viongozi) waongofu.
Mafunzo
Hapa kuna fadhila za wazi za Hassan na Hussein radhi za Allah ziwe juu yao.
Imesemekana katika maana ya hadithi kuwa: Wao wakati wa kuzungumzwa hadithi hii walikuwa ndio mabosi wa vijana wa wale miongoni mwao watakaokuwa katika watu wa peponi katika vijana wa zama hizi, au wao ni bora kuliko yule ambaye fadhila zake hazijathibiti kwa ujumla kama Manabii na Mahalifa (viongozi), au wao ni mabosi wa kila mwenye kusifika na sifa ya ujana, kama murua (heshima) na ukarimu na ushujaa, na haukutajwa umri maalumu wa ujana; kwa sababu Hassan na Hussein walikufa wakiwa watu wazima.
Marejeo
سنن الترمذي (6/ 113) (3768).
مسند أحمد (17/ 31) (10999).
حاشية السندي على سنن ابن ماجه، محمد بن عبد الهادي التتوي (1/ 56).
تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، محمد المباركفوري (10/ 178).
المصباح المنير في غريب الشرح الكبير، لأحمد الفيومي (1/ 294).
عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها أَنَّهَا قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: «مَا مِنْ مُسْلِمٍ تُصِيبُهُ مُصِيبَةٌ فَيَقُولُ مَا أَمَرَهُ اللهُ: {إِنَّا لِلهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ} [البقرة: 156]، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي، وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا، إِلَّا أَخْلَفَ اللهُ لَهُ خَيْرًا مِنْهَا»، قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ قُلْتُ: أَيُّ الْمُسْلِمِينَ خَيْرٌ مِنْ أَبِي سَلَمَةَ؟ أَوَّلُ بَيْتٍ هَاجَرَ إِلَى رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم، ثُمَّ إِنِّي قُلْتُهَا، فَأَخْلَفَ اللهُ لِي رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم.
Kutoka kwa Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo" Akasema: Alipofariki Abuu Salama, nikasema: Ni Muislamu gani atakuwa bora kuliko Abuu Salama? Nyumba ya kwanza aliyohamia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi nikasema maneno hayo, Mwenyezi Mungu akanipa mbadala wake ambaye ni Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza mama wa waumini Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema siku moja: Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyopendezeshewa na Mwenyezi Mungu kwake kuyasema: "Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea" [Baqara: 156], "Ewe Mwenyezi Mungu nilipe" na unipe malipo ya subira yangu "katika msiba wangu", na unipe badala "na unirejeshee" kwa hilo "kheri kuliko hiyo"; isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa mbadala bora kuliko hilo. Akasema: Alipofariki Abuu Salama akasema: Ni nani katika Waislamu atakuwa bora kuliko Abuu Salama?! Nyumba ya kwanza iliyohama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi Mwenyezi Mungu alinisaidia nikaisema kauli hiyo, Mwenyezi Mungu akanipa badala Mtume rehema na amani ziwe juu yake bora zaidi kuliko Abuu Salama.
Mafunzo
Amri ya kuwa na subira wakati wa mitihani masaibu na kutopaparika.
Kuelekeza dua kwa Mwenyezi Mungu katika mambo mazito; kwa sababu kwake ndio kuna mbadala.
Umuhimu wa waumini kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hata isipojulikana hekima yake.
Kheri yote kwa muumini iko katika kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com