Msiwatukane Maswahaba wangu, kwa sababu, lau kama yeyote kati yenu atatoa dhahabu sawa na (mlima) Uhud (katika njia ya Mwenyezi Mungu), basi haiwezi kuwa sawa na theluthi mbili ya kilo ya mmoja wao wala nusu yake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane Maswahaba wangu, kwa sababu, lau kama yeyote kati yenu atatoa dhahabu sawa na (mlima) Uhud (katika njia ya Mwenyezi Mungu), basi haiwezi kuwa sawa na theluthi mbili ya kilo ya mmoja wao wala nusu yake."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwatukana Maswahabah hasa wa mwanzo katika Muhajirina na Ansari; na akaeleza kuwa lau mmoja miongoni mwa watu angetoa dhahabu nyingi kama mlima Uhudi, zisingefikia thawabu zake kwa hilo malipo ya kibaba cha Swahaba mmoja au nusu yake - na kibaba ni kujaza viganja viwili vya mtu wa wastani-; Na hii ni kwa sababu ya ikhilas yao kuwa zaidi, na ukweli wa nia zao, na kuwahi kwao kutoa na kupigana kwao katika njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya ufunguzi wa mji wa Makka, ambapo uhitaji wake ulikuwa mkubwa.
Mafunzo
Kuwatukana Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ni haramu, na ni katika maasi makubwa.
Marejeo
صحيح البخاري (5/ 8) (3673).
صحيح مسلم (4/ 1967) (2540).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري، لبدر الدين العيني (16/ 187).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (16/ 93).
الإفصاح عن معاني الصحاح، ليحيى بن هبيرة (8/ 70).
نزهة النظر في توضيح نخبة الفكر في مصطلح أهل الأثر، لأحمد بن حجر العسقلاني (ص111).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com