Kutoka kwa Abuu Humaid Assaaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.