Ruka hadi kwenye maudhui
Sahih al-Bukhari

Na. 6780

Na. 6780Kitabu cha 86, na. 9
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، قَالَ حَدَّثَنِي خَالِدُ بْنُ يَزِيدَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِلاَلٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ، أَنَّ رَجُلاً، عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم كَانَ اسْمُهُ عَبْدَ اللَّهِ، وَكَانَ يُلَقَّبُ حِمَارًا، وَكَانَ يُضْحِكُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم قَدْ جَلَدَهُ فِي الشَّرَابِ، فَأُتِيَ بِهِ يَوْمًا فَأَمَرَ بِهِ فَجُلِدَ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الْقَوْمِ اللَّهُمَّ الْعَنْهُ مَا أَكْثَرَ مَا يُؤْتَى بِهِ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ لاَ تَلْعَنُوهُ، فَوَاللَّهِ مَا عَلِمْتُ أَنَّهُ يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ‏"‏‏.‏
Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja alikuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake jina lake anaitwa Abdallah, na alikuwa akitaniwa kwa jina la Punda, na alikuwa akimchekesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa viboko kwa sababu ya ulevi, basi akaletwa siku moja akaamrisha akachapwa, akasema mtu mmoja katika jamaa waliopo: Ewe Mwenyezi Mungu mlaani, ni mara ngapi analetwa!? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake".

Tafsiri: HadeethEnc.comMaelezo yake

Chanzo hakirekodi daraja lolote kwa hadithi hii.

Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.

Kitabu cha 86 · Limits and Punishments set by Allah (Hudood)

Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.