Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.