Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.