Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Kiongozi muadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika misikiti, na watu wawili walipoendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakakutana kwa ajili yake na wakaachana kwa ajili yake, na mwanaume aliyeitwa na mwanamke mwenye wadhifa na uzuri, akasema: Hakika mimi ninamhofu Allah, na mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka usijue kushoto kwake unachotoa kulia kwake, na mtu aliyemkumbuka Mwenyezi Mungu akiwa faragha, yakabubujika machozi macho yake".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.