حَدَّثَنَا عَبْدَانُ، قَالَ أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، قَالَ أَخْبَرَنَا يُونُسُ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، ح وَحَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ مُحَمَّدٍ، قَالَ أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، قَالَ أَخْبَرَنَا يُونُسُ، وَمَعْمَرٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، نَحْوَهُ قَالَ أَخْبَرَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَجْوَدَ النَّاسِ، وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ، وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ، فَلَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَجْوَدُ بِالْخَيْرِ مِنَ الرِّيحِ الْمُرْسَلَةِ.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili, na alikuwa akikutana naye katika kila usiku wa Ramadhani akimsomesha Qur'ani, basi hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na Amani ziwe juu yake- ni mkarimu zaidi kwa mambo ya kheri kuliko hata upepo uliotumwa.
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.