Al-Qadr
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِنَّآ أَنزَلْنَـٰهُ فِى لَيْلَةِ ٱلْقَدْرِ 1
{1} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha ubora wa Qur-ani na daraja yake ya juu: "Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani katika Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu)." [Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa."] Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alianza kuteremsha Qur-ani katika mwezi wa Ramadhani katika usiku wa huu wa Cheo, na Mwenyezi Mungu akawarehemu waja wake kwa rehema za jumla, ambazo waja hawawezi kuzishukuru. Na imeitwa Laylat al-Qadr kutokana na cheo chake kikubwa na ubora wake mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwa sababu Yeye hupitisha ndani yake kitakachotokea katika mwaka mzima miongoni mwa umri mbalimbali, riziki, mipango mbalimbali ya kimungu.