Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sura ya 9

At-Tawba

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 4

إِلَّا ٱلَّذِينَ عَـٰهَدتُّم مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنقُصُوكُمْ شَيْـًٔا وَلَمْ يُظَـٰهِرُوا۟ عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوٓا۟ إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ 4

{4} Yaani, kujiweka mbali huku kamili na kusikokuwa na kipimo dhidi ya washirikina wote, "Isipokuwa wale mlioahidiana nao katika washirikina" na wakaendelea na agano lao, na hakuna kitu kilichofanyika kutoka kwao kinachohitaji kulivunja. Hawakuwapunguza kitu wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi hawa watimizieni agano lao mpaka muda wao, sawa ni mchache au mwingi. Kwa sababu Uislamu hauamrishi hiana, bali unaamuru kutimiza. "Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wachamungu," ambao wanafanya yale waliyoamrishwa, na wakajiepusha na shirki, na hiana, na mengineyo miongoni mwa madhambi.