Al-Inshiqaaq
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ 7 فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا 8 وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا 9
{7 - 9} Ndiyo maana akataja malipo hayo kwa undani akisema: "Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia" na hao ndio watu wa furahani, "Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi." Ambayo ni kuonyeshwa kwepesi mbele ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu amfanye kukubali madhambi yake, mpaka mja atakapodhani kwamba ameangamia, Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Hakika mimi nimekufichia hayo katika dunia, na tena ninakufichia hayo hivi leo "Na arudi kwa ahali zake" Peponi "kwa furaha" kwa sababu ameepushwa na adhabu na akapata malipo mazuri.