Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Muddaththir
Sura ya 74

Al-Muddaththir

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 35–37

إِنَّهَا لَإِحْدَى ٱلْكُبَرِ 35 نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ 36 لِمَن شَآءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ 37

{35 - 37} Na kile kilichoapiwa ni kauli yake: "Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!" Kwa hivyo, tukikujulisheni juu yake na mkajua vyema jambo lake, basi anayetaka kutangulia miongoni mwenu na kufanya yatakayomweka karibu na Mwenyezi Mungu na kumsogeza karibu mno na radhi zake na nyumba ya utukufu wake, au anayetaka akabaki nyuma katika kile alichoumbwa kwa ajili yake na kile anachokipenda Mwenyezi Mungu na kukiridhia, basi na afanye maasi na ajiweke karibu na Jahannam. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye aamini..." hadi mwisho wa Aya.