Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Jinn
Sura ya 72

Al-Jinn

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 21–22

قُلْ إِنِّى لَآ أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا 21 قُلْ إِنِّى لَن يُجِيرَنِى مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلْتَحَدًا 22

{21 - 22} "Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni" Kwani mimi ni mja, wala sina chochote katika kuamrisha na kuendesha mambo. "Sema: Hakika hapana yeyote awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu" ambaye ataweza kuniokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa Mtume, ambaye ni mkamilifu zaidi wa viumbe wote, hawezi kumiliki madhara wala uwongofu, na wala hawezi kujizuia chochote kutokana na Mwenyezi Mungu akimtakia mabaya, basi asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe ndio wanafailia zaidi na kustahili zaidi kutokuwa na uwezo huo, "wala sitapata pa kukimbilia isipokuwa kwake Yeye tu."