Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qalam
Sura ya 68

Al-Qalam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 5–6

فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ 5 بِأَييِّكُمُ ٱلْمَفْتُونُ 6

{5 - 6} Mwenyezi Mungu alipomteremsha kwenye vituo vya juu kabisa [kwa namna zote], na maadui zake walikuwa wakidai kwamba yeye ni mwendawazimu na amepumbazika, akasema: “Karibu utaona, na wao wataona. Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu." Na tayari ilibainika kuwa yeye ndiye mwongofu na mkamilifu zaidi katika watu wote, yeye mwenyewe na kuwafanyia hivyo wengine, na kwamba maadui zake ndio watu wapotovu zaidi na waovu kwa watu, na kwamba wao ndio waliowatia majaribuni waja wa Mwenyezi Mungu na kuwapoteza mbali na njia yake, na elimu ya Mwenyezi Mungu juu ya hilo inatosha kabisa. Kwa maana Yeye ndiye atakayewafanyia hesabu viumbe juu ya matendo yao, Mlipaji.