As-Saff
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰٓ إِلَى ٱلْإِسْلَـٰمِ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ 7
{7} “Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo” kama huu au mwingineo, ilhali hana udhuru wowote, na tayari hoja zake zilikwisha katika, kwa sababu “anaitwa kwenye Uislamu” na anabainishiwa hoja zake na ushahidi wake ulio wazi. “Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.” Wale wanaoendelea kung'ang'ania katika dhuluma yao, ambao hakuna mawaidha yanayoweza kuwarudisha wala hawakemewi na ubainisho wala hoja, hasa madhalimu hawa wanaosimama kidete kukabiliana na haki ili kuikataa na kuinusuru batili.