Al-Maaida
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
قَالُوا۟ يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا۟ مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا۟ مِنْهَا فَإِنَّا دَٰخِلُونَ 22
{22} Basi wakasema maneno yanayoashiria udhaifu wa nyoyo zao, na udhaifu wa nafsi zao, na kutojali kwao amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. "Ewe Musa! Hakika, huko wako watu majabari" wenye nguvu nyingi na ujasiri. Yaani, hili ni katika vizuizi kwetu kuingia humo, "Nasi kamwe hatutaingia humo mpaka wao watoke humo. Wakitoka humo, hapo hakika tutaingia." Na Haya ni katika na woga na kukosa yakini, vinginevyo; lau wangekuwa na akili yao timamu, Wangejua kwamba wao wote ni wanadamu, na kwamba mwenye nguvu ni yule anayesaidiwa na Mwenyezi Mungu kwa nguvu kutoka Kwake. Kwa maana hakuna hila wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, na ili wajue kwamba watanusuriwa juu yao kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaahidi hilo ahadi maalumu.