Al-Ghaafir
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَإِذْ يَتَحَآجُّونَ فِى ٱلنَّارِ فَيَقُولُ ٱلضُّعَفَـٰٓؤُا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا نَصِيبًا مِّنَ ٱلنَّارِ 47
{47} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu watu wa Motoni, kuzozana kwao wenyewe kwa wenyewe, kulaumiana kwao,kutafuta kwao msaada kutoka kwa Mlinzi wa Moto na kutokuwa na manufaa yoyote katika kuomba kwao huko. Alisema: "Na watakapohojiana huko Motoni," wafuasi wataweka ushahidi kwamba walidanganywa na wale ambao wao waliwafuata, lakini hao waliofuatwa watajitenga mbali na hao waliowafuata. "Wanyonge watawaambia wale waliojitukuza" na wakawalingania katika yale waliyokuwa wakiyafanyia kiburi: "Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu." Mlitupoteza na mkatupambia ushirikina na uovu. "Basi je, hamtuondolei sehemu ya huu Moto?"