Al-Ghaafir
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
يَوْمَ تُوَلُّونَ مُدْبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ ۗ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنْ هَادٍ 33
{33} Yeye, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, akawahofisha juu ya siku hii mbaya zaidi, na akaona uchungu juu yao ikiwa wataendelea na ushirikina wao huo. Ndiyo maana akasema: "Siku mtakapogeuka kurudi nyuma" wakati mnapelekwa Motoni. "Hamtakuwa na wa kukulindeni kutokana na Mwenyezi Mungu," wala nyinyi wenyewe hamtakuwa na nguvu ya kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu "Siku zitakapodhihirishwa siri. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi." "Na mwenye kupotezwa na Mwenyezi Mungu, basi huyo hana wa kumwongoa." Kwa sababu uwongofu uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu tu. Ikiwa atamnyima mja wake uwongofu kwa sababu anajua kuwa haufailii huo kwa sababu ya uovu wake, basi hakuna njia yoyote ya kumuongoa huyo.