Al-Ghaafir
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَقَالَ ٱلَّذِىٓ ءَامَنَ يَـٰقَوْمِ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُم مِّثْلَ يَوْمِ ٱلْأَحْزَابِ 30
{30} "Na akasema yule aliyeamini" akirudia kuwalingania kaumu yake bila kukata tamaa na kuongoka kwao. Hivi ndivyo ilivyo hali ya wale wanaolingania kwa Mwenyezi Mungu. Wanaendelea kulingania kwa Mola wao Mlezi, na hakuna chochote kinachoweza kuwazuia kufanya hivyo, na wala kiburi cha yule wanaowalingania hakiwakatishi tamaa ya kurudia wito. Aliwambia: "Enyi watu wangu! Hakika mimi nakuhofieni mfano wa siku za makundi." Yaani, umma waliokadhibisha ambao walijipanga makundi dhidi ya Manabii wao na wakakusanyika ili kuwapinga.