Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ghaafir
Sura ya 40

Al-Ghaafir

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 21–22

أَوَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ كَانُوا۟ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا۟ هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَءَاثَارًا فِى ٱلْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٍ 21 ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَكَفَرُوا۟ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ قَوِىٌّ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ 22

{21-22} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Kwani hawatembei katika ardhi" kwa mioyo yao na miili yao, kwa njia ya kuzingatia na kutafakari juu ya athari mbalimbali, kwa hivyo wakaangalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa wale waliokuwa wakikadhibisha? Wataukuta kwamba ulikuwa mbaya zaidi, kwa kuwa waliangamizwa, wakatiwa hizaya, wakafedheheshwa, ilhali hapo awali walikuwa na nguvu kuliko hawa kwa idadi, maandalizi, ukubwa wa miili "na athari katika nchi" kwa ujenzi na upandaji mimea. "Na Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao" walipozikakamia na kuendelea kuzifanya. "Bila ya shaka Yeye ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu." Nguvu zao hizo hazikuwa na manufaa mbele ya nguvu za Mwenyezi Mungu. Bali miongoni mwa kaumu waliokuwa na nguvu zaidi, walikuwa kaumu ya 'Aad, ambao walisema: "Ni nani mwenye nguvu kutushinda sisi?" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawatumia upepo uliodhoofisha nguvu zao hizo na ukawaangamiza wote kabisa.