Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sura ya 39

Az-Zumar

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 44

قُل لِّلَّهِ ٱلشَّفَـٰعَةُ جَمِيعًا ۖ لَّهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ 44

{44} "Sema" ukiwaambia "Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu," kwa sababu mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu na kila muombezi anamhofu, na wala hakuna anayeweza kufanya uombezi kwake isipokuwa kwa idhini yake. Akitaka kumrehemu mja wake anamruhusu mwombezi mtukufu kwake amfanyie uombezi kwa sababu ya kuwarehemu wote wawili. Kisha akathibitisha kwamba uombezi wote ni wake, kwa kauli yake: "Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi" pamoja na vyote vilivyomo [ndani yake] kama vile dhati mbalimbali, vitendo na sifa. Basi la lazima ni kuomba uombezi kutoka kwa Yule anayeumiliki na kumfanyia Yeye peke yake ibada. "Kisha mtarejeshwa kwake." Naye atamlipa mwenye kumkusudia Yeye tu ujira mkubwa, na amlipe anayemshirikisha kwa adhabu kali.