Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Saad
Sura ya 38

Saad

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 44

وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَٱضْرِب بِّهِۦ وَلَا تَحْنَثْ ۗ إِنَّا وَجَدْنَـٰهُ صَابِرًا ۚ نِّعْمَ ٱلْعَبْدُ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ 44

{44} "Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo." Wafasiri walisema: Wakati wa maradhi yake na dhiki yake hii, alikuwa amemkasirikia mkewe katika baadhi ya mambo, kwa hivyo akaapa kwamba Mwenyezi Mungu akimponya, lazima atampiga mijeledi mia moja. Basi Mwenyezi Mungu alipomponya, na mkewe huyo alikuwa mwema na alikuwa akimfanyia uzuri. Mwenyezi Mungu akamrehemu mkewe huyu na pia akamrehemu Ayubu. Kwa hivyo akamtolea hukumu kwamba ampige kwa kicha cha vijiti mpigo mmoja tu, na kwa hilo atakuwa ameshatimiza kiapo chake. "Hakika tulimkuta ni mwenye subira." Ambapo tulimpa mtihani wa balaa kubwa, lakini akavumilia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. "Mbora wa waja," kwani alikamilisha viwango vya kumuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati nzuri na nyakati mbaya, katika dhiki na wepesi. "Kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu," na kumrudia Mwenyezi Mungu katika matakwa yake ya kidini na ya kidunia. Na alikuwa mwingi wa kumtaja Mola wake Mlezi, mwingi wa kumuomba dua, mwenye upendo mkubwa kwake, na mwingi wa kumfanyia Yeye tu uungu.