Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · As-Saaffaat
Sura ya 37

As-Saaffaat

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 63–66

إِنَّا جَعَلْنَـٰهَا فِتْنَةً لِّلظَّـٰلِمِينَ 63 إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِىٓ أَصْلِ ٱلْجَحِيمِ 64 طَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَـٰطِينِ 65 فَإِنَّهُمْ لَـَٔاكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ 66

{63 - 66} "Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa waliodhulumu" kwa ukafiri na maasi. "Hakika huo ni mti unaotoka katikati ya Jahannamu," ambapo ndiyo chanzo chake, chanzo kibaya zaidi na kupanda kuovu zaidi kunakoashiria uovu, kilichopandwa na uduni wake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akatutanabahisha uovu wake kwa kutaja mahali unapomea, na kwa kututajia katika maelezo ya matunda yake, kwamba ni kama vichwa vya mashetani. Basi baada ya hayo, usiulize juu ya ladha yake na kile ambacho unafanya ndani ya miili yao na katika matumbo yao. Hawawezi kuuwacha wakaenda kwingine. Ndiyo maana akasema: "Basi hakika bila ya shaka hao watakula kwayo, na wajaze matumbo." Hiki ndicho chakula cha wakazi wa Motoni; chakula kibovu zaidi ni chakula chao hiki.