Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · As-Saaffaat
Sura ya 37

As-Saaffaat

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 151–157

أَلَآ إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ 151 وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ 152 أَصْطَفَى ٱلْبَنَاتِ عَلَى ٱلْبَنِينَ 153 مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ 154 أَفَلَا تَذَكَّرُونَ 155 أَمْ لَكُمْ سُلْطَـٰنٌ مُّبِينٌ 156 فَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ 157

{151 - 157} Ndiyo maana akasema: "Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo! Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wa kiume? Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi," kwa hukumu hii ya udhalimu? "Basi je, hamkumbuki" mkaipambanua kauli hii batili yenye dhuluma? Kwani kama mngekumbuka, basi hamngesema kauli hii. "Au mnayo hoja iliyo wazi" juu ya kauli yenu hii kutoka kwa kitabu au Mtume? Lakini haya yote hayakuwa, ndiyo maana akasema: "Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli." Kwa maana, mwenye kusema kauli ambayo hana ushahidi wa kisheria juu yake, basi yeye ni mwongo wa makusudi au anazungumza juu ya Mwenyezi Mungu bila elimu.