Yaseen
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا مَنۢ بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا ۜ ۗ هَـٰذَا مَا وَعَدَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ ٱلْمُرْسَلُونَ 52
{52} Katika hali hiyo wale waliokadhibisha watahuzunika na kujuta, na watasema: "Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu?" Yaani, jumo makaburini. Kwa sababu ilisimuliwa katika baadhi ya hadithi kwamba watu wa makaburini watalala kulala fulani muda mfupi tu kabla ya kupulizwa katika baragumu. Wataitikiwa na waambiwe: "Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume." Na leo yamekuwa kweli mnayaona kwa macho. Wala usidhani kuwa kutajwa kwa Mwingi wa Rehema mahali hapa ni kujulisha tu kuhusu ile ahadi yake. Bali ni kufahamisha kwamba siku hiyo kuu wataona rehema yake kwa namna ambayo haikuwahi kuwapitia akilini mwao wala wenye kutarajia hawakuwahi kutarajia. Kama vile kauli yake: "Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman (Mwingi wa Rehema)." Na kauli yake, "Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani Mwingi wa Rahema." Na mfano wa hayo ambapo jina lake 'Arrahmani (Mwingi wa rehema)' limetajwa.