Ar-Room
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَـٰنًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا۟ بِهِۦ يُشْرِكُونَ 35
{35} "Au tumewateremshia hoja" iliyo dhahiri. Basi hiyo" hoja "inazungumza juu ya kile walichokuwa wakishirikisha nacho?" Na inawaambia: Kuweni imara juu ya ushirikina wenu na endeleeni kuwa na shaka; kwani mliyo juu yake ndiyo Haki, na yale waliyowaitia Mitume ni batili. Basi je, wanayo hoja hiyo ambayo inawafanya kushikamana sawasawa na ushirikina? Ama ushahidi wa kiakili wote na wa kusikia, na vitabu vya mbinguni, na Mitume watukufu, na mabwana wa wanadamu, walikataza kabisa jambo hili, na wakatahadharisha juu ya kufuata njia zake zinazofikisha huko, na wakahukumu kuwa akili na dini ya mwenye kufanya hivyo ni mbovu? Basi ushirikina wa watu hawa hauna hoja yoyote wala uthibitisho, bali ni matamanio tu ya nafsi na uchochezi wa Shetani.