Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ankaboot
Sura ya 29

Al-Ankaboot

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 49

بَلْ هُوَ ءَايَـٰتٌۢ بَيِّنَـٰتٌ فِى صُدُورِ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَّا ٱلظَّـٰلِمُونَ 49

{49} Yaani, Qur-ani hi,i "ni Ishara zilizo wazi" hazina chochote kilichofichika "katika vifua vya wale waliopewa elimu." Nao ni mabwana wa viumbe na wenye akili nzuri miongoni mwao, waliokamilika. Kwa hivyo, ikiwa ni aya zilizo wazi katika vifua vya watu kama hao, basi wao ni hoja dhidi ya wengineo. Na kukanusha kwa wengineo hakudhuru, na wala hilo haliwi isipokuwa dhuluma tu. Na ndiyo maana akasema, "Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa madhalimu." Kwa sababu hazikatai isipokuwa asiyejua, ambaye kazungumza bila elimu, wala hakuwafuata wanazuoni. Naye ima ana udhabiti juu ya uhakika wake, ai anajifanya kuwa mjinga, alijua kuwa hiyo ndiyo haki lakini akakaidi tu, na akajua kuwa ni ukweli, lakini akauhalifu tu.