An-Naml
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ 71
{71} Na wanasema hao wanaokadhibisha ufufuo na haki ambayo Mtume alikuja nayo huku wakiifanyia pupa adhabu, "Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?" Na hili ni kutokana na upumbavu wa maoni yao na ujinga wao, kwa sababu Mwenyezi Mungu amekuwekea kutokea kwake na wakati na muda maalumu; kwa hivyo kutokuja kwake haraka, hakuonyeshi baadhi ya matashi yao, lakini pamoja na hili, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, akiwaonya juu ya kutokea kwa kile wanachokifanyia haraka: