An-Naml
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ 3
{3} Labda inaweza semwa: Labda kuna watu wengi ambao wanadai kwamba wameamini. Je, itakubalika kutoka kwa kila mmoja anayedai kuwa anayaamini hayo? Au lazima hilo liwe na ushahidi, na hilo ndilo la haki? Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha sifa ya waumini, akasema, "Ambao wanashika Swala" za faradhi zake, na za sunna zake. Wanatekeleza matendo yake ya dhahiri kama vile nguzo zake, masharti yake, wajibu zake [bali], hata yale yanayopendekezwa kufanya ndani yake, na pia matendo yake ya ndani, kama vile kunyenyekea ambako ndiko roho yake na kiini chake; kwa kuhisi ukaribu wa Mwenyezi Mungu na kutafakari yale ambayo mtu anayeswali anayasema na kufanya. "Na wanatoa Zaka" ya faradhi kuwapa wale wanaostahili kupewa. "Na Akhera wana yakini nayo;" yaani, imani yao imefikia daraja la kuwa na yakini, ambayo ni elimu kamili yenye kutoka moyoni mwa mwenye kuomba hadi katika matendo. Na yakini yao juu ya Akhera inalazimu ukamilifu wa kufanya kwao juhudi kuifikia, na akawatahadharisha juu ya sababu za adhabu na mambo yenye kuisababisha. Na hii ndiyo asili ya heri yote.