Al-Muminoon
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَٰتِ ٱلشَّيَـٰطِينِ 97 وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ 98
{97-98} Ama yule ambaye kwamba ni muovu kutokamana na mashetani; hufaidika na wema, wala halinganii kundi lake isipokuwa wawe miongoni mwa watu wa motoni; basi katika jambo la muhimu katika kukabiliana naye, ajiongoze katika uongozi ambao alimwongoza Mwenyezi Mungu mtume wake. Na akasema "Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako;" (yaani, najilinda kwa hila zako na nguvu zako na kujieka mbali na hila zangu na nguvu)," na wasiwasi wa mashetani. "Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie;" yaani, najilinda kwako kutokana na shari itakayonipata kwa sababu ya kutangamana nao na wasiwasi wao na mguso wao, na kutokana na shari ambayo ni kwa sababu ya kuhudhuria kwao na wasiwasi wao, na dua hii ya kujilinda ni kutokana na kila lenye shari na asili yake, na yaingia katika kila kujikinga na kila mvutano wa shetani na mguso wake na wasiwasi wake. Basi pindi akimkinga Mwenyezi Mungu mja wake kutokana na shari hii, na akajibu dua yake; atasalimika kutokana na kila shari, na atawafikika katika kila heri.