Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sura ya 21

Al-Anbiyaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 30

أَوَلَمْ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَـٰهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ ٱلْمَآءِ كُلَّ شَىْءٍ حَىٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ 30

{30} Yaani, je, hawaoni hawa waliomkufuru Mola wao Mlezi, na wakakataa kumtatakasia ibada yenye kuwaonyesha kwamba ishara na kushuhudia kwamba Yeye ndiye Mola Mlezi Msifiwa. Kwa hivyo wakaziona mbingu na ardhi na wakazikuta kwamba "zilikuwa zimeambatana" kwa namna ya kwamba hii (mbingu) haikuwa na mawingu wala mvua, na hii (ardhi) ilikuwa imetulia, maiti bila ya ya mmea wowote ndani yake. "Kisha Sisi tukazibandua" mbingu kwa mvua, na ardhi kwa mimea. Je, Yeye si yule aliyetia mawingu angani baada ya kwamba hali ya hewa ilikuwa shwari bila ya mawingu yoyote, na akatia humo maji mengi, kisha akayapeleka kwenye nchi iliyokufa, iliyojaa mavumbi katika pande zake, na maji yake yakawa yamekauka, kwa hivyo akaifanya kunyesha huko, basi ikatetemeka, ikasonga, na ikasisimka na kututumka na ikaotesha katika mimea ya kila namna nzuri, yenye kutofautiana sampuli zake, yenye faida nyingi? Je, hayo si ushahidi kwamba yeye ndiye wa kweli, na kisichokuwa yeye ni batili, na kwamba atawahuisha wafu, na kwamba yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu? Na ndiyo maana akasema, "Basi je, hawaamini" imani sahihi isiyokuwa na shaka yoyote wala ushirikina?