Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sura ya 21

Al-Anbiyaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 16

وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَـٰعِبِينَ 16

{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba hakuumba mbingu na ardhi bure au kwa mchezo bila ya faida yoyote. Bali aliziumba kwa haki na kwa ajili ya haki, ili waja waweze kuvitumia kama ushahidi kwamba Yeye ndiye Muumba Mkuu, Mwendeshaji mambo Mwenye hekima, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu, ambaye ana ukamilifu wote, na sifa zote, na utukufu wote, Mkweli katika usemi wake, ambaye Mitume wake ni wakweli katika yale wanayojulisha kumhusu. Na kwamba anaweza kuviumba pamoja na upana wake na ukubwa wake, na anaweza kurudisha miili baada ya mauti yake, ili amlipe mzuri kwa uzuri wake, na mbaya kwa ubaya wake.