Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Taa-Haa
Sura ya 20

Taa-Haa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 89

أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا 89

{89} Hili ni kutokana na ugumu wa kufahamu kwao na upumbavu wa akili zao, walipoona kitu hiki kigeni ambacho kilianza kutoa mlio wa ng'ombe baada ya kwamba kilikuwa hakina uhai, kwa hivyo wakamdhania kwamba yeye ndiye mungu wa ardhi na mbingu. Je, hawaoni kwamba ndama huyo "hakuwarudishia neno?" Yaani, haongei na kujadiliana nao, ''wala kuwamilikia kudhuru wala kufaa?" Kwa hivyo, asiyekuwa mkamilifu, ambaye hawezi kuongea na kutenda hastahili kuabudiwa. Naye ni mwenye upungufu zaidi ya wale wanaomuabudu. Kwa maana wao wanazungumza na wanaweza baadhi ya vitu kama vile kunufaisha na kuzuia kupitia Mwenyezi Mungu kuwapa uwezo juu ya hayo.