Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 49–54

وَإِذْ نَجَّيْنَـٰكُم مِّنْ ءَالِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوٓءَ ٱلْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَآءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَآءَكُمْ ۚ وَفِى ذَٰلِكُم بَلَآءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ 49 وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ ٱلْبَحْرَ فَأَنجَيْنَـٰكُمْ وَأَغْرَقْنَآ ءَالَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ 50 وَإِذْ وَٰعَدْنَا مُوسَىٰٓ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ ٱتَّخَذْتُمُ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِهِۦ وَأَنتُمْ ظَـٰلِمُونَ 51 ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ 52 وَإِذْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ 53 وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِٱتِّخَاذِكُمُ ٱلْعِجْلَ فَتُوبُوٓا۟ إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَٱقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ 54

(49-54) Huu ndio mwanzo wa kubainisha neema zake (Mwenyezi Mungu) juu ya Wana wa Israili kwa undani. Akasema: "Na vile tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Firauni." Yani kutoka kwa Firauni na wakuu wake na majeshi yake. Na walikuwa kabla ya hapo "waliokupeni" yani kuwatumia na kuwapa "adhabu mbaya" yani kali sana. "Wakiwachinja wana wenu wa kiume" kwa kuogopa kuongezeka kwenu. "Na wakawawacha hai wanawake" yani hawakuwa wakiwaua. Basi mkawa kati ya wanaouawa na wale wanaodhalilishwa kwa kazi ngumu, wanaoachwa kuishi kwa njia ya hisani na kutawaliwa. Basi huku ndiko kudhalilishwa kwa juu mno. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa uokozi kamili, na kumzamisha adui yao hali ya kuwa wanatazama ili macho yao yafurahike "katika hayo" yani kuwaokoa "ulikuwa (uokozi huo) ni ihsani kubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Kwa hivyo, hayo ndiyo yanayowalazimu nyinyi kushukuru na kutekeleza maamrisho yake. Kisha akawatajia neema yake juu yao ya kumwahidi Musa usiku arubaini; ili awateremshie Taurati iliyojumuisha neema kubwa na masilahi ya jumla. Kisha wao hawakungoja mpaka kukamilika kwa miadi hiyo mpaka wakamwabudu ndama nyuma ya kuondoka kwake (Musa). "Na mkawa wenye kudhulumu" huku mkijua dhuluma yenu, na hoja imekwishathibitika juu yenu. Hilo ni kosa kubwa mno na dhambi kubwa sana. Kisha akakuamrisheni kutubu juu ya ulimi wa Nabii wake Musa kwa kuuana nyinyi kwa nyinyi, basi Mwenyezi Mungu akakusameheni kwa sababu ya hayo "ili mpate kushukuru" Mwenyezi Mungu.