Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَقَـٰتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يُقَـٰتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْمُعْتَدِينَ 190
Aya hizi zinajumuisha amri ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na hili lilikuwa baada ya kuhamia Madina, wakati Waislamu walipokuwa na nguvu za kupigana, Mwenyezi Mungu akawaamrisha kufanya hivyo, baada ya kwamba walikuwa wameamrishwa waizuie mikono yao. Na katika kukuzuia kupigana “katika njia ya Mwenyezi Mungu” kuna kuhimiza watu kuwa na ikhlasi; na kukataza kupigana katika kufitinisha baina ya Waislamu. “Wale wanaopigana nanyi,” yani ambao wako tayari kupigana na nyinyi, nao ni wanaume wa umri wa kuamrishwa na kukatazwa na sio wazee ambao hawana maoni wala uwezo wa kupigana. Na kukataza kuanzisha uadui kunajumuisha aina zote za kuanzisha uchokozi, kama vile kuua asiyepigana kama vile wanawake, vichaa, watoto, watawa na wengineo. Na kukatakata wale waliouawa, kuua wanyama, kukata miti [na mengineyo], bila ya kuwepo masilahi yanayowarudia Waislamu. Na katika kuanzisha uadui ni kupigana na wale ambao jizya inakubaliwa kutoka kwao wanapoitoa, kwa sababu hilo haliruhusiki.