Yusuf
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
يَـٰصَـٰحِبَىِ ٱلسِّجْنِ ءَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ 39
{39} Kisha akawalingania kwa uwazi, akasema: "Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi tofautitofauti ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu?" Yaani, je, mabwana wasio na uwezo na walio dhaifu ambao hawanufaishi wala hawadhuru wala hawapeani wala hawanyimi, nao wametofautiana kama vile miti, mawe, Malaika, wafu na aina nyinginezo za miungu wanayoichukua washirikina? Je, hao ndio bora au Mwenyezi Mungu ambaye ana sifa za ukamilifu, mmoja kwa dhati yake, na sifa Zake, na matendo Yake? Na Yeye hana mshirika yoyote katika lolote miongoni mwa hayo, Mwenye nguvu, ambaye vitu vyote viko chini ya nguvu zake na mamlaka yake. Kwa hivyo, chochote anachotaka, kinakuwa. Na asichotaka, hakiwi. hakuna mnyama yeyote isipokuwa amekikamata kwa nywele za mbele ya kichwa chake.