La yukallifu Allahu nafsan illa wusAAaha laha ma kasabat waAAalayha ma iktasabat rabbana la tuakhithna in naseena aw akhtana rabbana wala tahmil AAalayna isran kama hamaltahu AAala allatheena min qablina rabbana wala tuhammilna ma la taqata lana bihi waoAAfu AAanna waighfir lana wairhamna anta mawlana faonsurna AAala alqawmi alkafireena
Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kiwango cha iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia. (Semeni) Mola wetu Mlezi! Usituchukulie ubaya tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi! Usitutwike tusiyoyaweza, na uyatupilie mbali mabaya yetu, na utusamehe na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center · QuranEnc.com · version 1.0.5. Matamshi ni yale yanayosambazwa na Tanzil. Sabīl haijapitia lolote kati ya hayo.
Imeonyeshwa kamili, kutoka Qur’ani 2:286. Katika chapa maandishi haya ni mafupi zaidi. Mistari ya chapa iliyo hapa chini iliandikwa kwa maandishi mafupi.