Al-An'aam
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَلَا تَطْرُدِ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِٱلْغَدَوٰةِ وَٱلْعَشِىِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُۥ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَىْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَىْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ 52
{52} "Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka uso wake." Yaani, usiwafukuze wakuondokee na kutoka katika kukaa pamoja nawe wale wafanyao ibaada, na wenye ikhlasi kwa kutaka kukaa pamoja na wasiokuwa wao, miongoni mwa wale wanaoshikamana na kumuomba Mola wao Mlezi kwa maombi ya ibada kwa dhikri , na Swala, na mfano wake; na dua ya kutaka kitu katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, hali ya kuwa wanakusudia kwa hayo uso wa mwenyezi Mungu; na hawana makusudio mengine isipokuwa kusudi hilo tukufu. Basi hawa hawastahiki kufukuzwa na kupewa mgongo. Bali wanastahiki kuwafanya marafiki wandani, na kuwapenda, na kuwasongea, na kuwaleta karibu zaidi. Kwa sababu, wao ndio wateule miongoni mwa viumbe - hata kama ni masikini – wao ni watukufu katika hali halisi, hata kama wao wanadhalilishwa na watu. "Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo." Yaani, kila mmoja ana hisabu yake, na ana matendo yake mema na matendo yake mabaya, "hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu." Na hakika yeye Nabii - swalah ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie - alitekeleza amri hii vikubwa kabisa. Basi akawa wanapoketi masikini miongoni mwa Waumini, anajisubirisha pamoja nao, na anaamiliana nao kwa uzuri, na anawawia laini, na anawaonyesha tabia nzuri, na akawasogeza karibu naye, bali wao walikuwa ndio wengi wa wale waliokuwa katika mkusanyiko wake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Na ilikuwa Sababu ya kuteremka kwa Aya hizi ni kwamba watu miongoni mwa Maquraishi au miongoni mwa Waarabu walimwambia Nabii - rehema na amani zimshukie:- ikiwa unataka tukuamini wewe na tukufuate, basi mfukuze fulani na fulani – watu miongoni mwa Maswahaba masikini; - kwani sisi hakika tunaona aibu Waarabu kutuona hali ya kuwa tumekaa pamoja na hawa watu masikini. Kwa hivyo, akabebwa na kupenda kwake kuwaona wakisilimu na kumfuata kwao, basi nafsi yake ikamwambia kuhusu hilo, lakini mwenyezi Mungu akamlaumu kwa aya hizi na mfano wake.