An-Nisaa
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
لَّـٰكِنِ ٱللَّهُ يَشْهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلْمِهِۦ ۖ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا 166
{166} Ilipotajwa kuwa Mwenyezi Mungu aliteremsha wahyi kwa Mtume wake Muhammad -rehema na amani zimshukie - kama alivyowateremshia ndugu zake miognoni mwa Mitume. Akajulisha hapa juu ya kushuhudia kwake Yeye mtukufu juu ya utume wake na usahihi wa yale aliyokuja nayo. Na kwamba, "Aliyateremsha kwa elimu." Inawezekana kuwa yaliyokusudiwa ni, aliyateremsha hali ya kuwa yamejumuisha elimu Yake. Yaani, yenye elimu ya kimwenyezi Mungu, na hukumu za kisheria, na habari za kighaibu ambazo ni katika elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo aliwafundisha waja wake. Na inawezekana kuwa yaliyokusudiwa ni, Aliyateremsha kutokana na elimu yake, na inakuwa katika hilo ishara na tanabihi juu ya ushahidi wake, na kwamba maana yake ni kwamba ikiwa Yeye Mtukufu aliiteremsha Qur-ani hii iliyojumuisha maamrisho na makatazo hali ya kuwa analijua hilo, basi anaijua hali ya aliyeiteremsha juu yake, na kwamba aliwalingania watu kwa hiyo. Kwa hivyo, mwenye kumuitikia, anamsadiki na anakuwa rafiki yake. Na mwenye kukakadhibisha na akamfanyia uadui, basi anakuwa adui yake, na akahalalisha mali yake na damu yake. Na Mwenyezi Mungu anampa uwezo, na anafuatanisha nusura yake, na anajibu maombi yake, na awaangusha maadui zake, na anawanusuru marafiki zake. Basi Je, kuna ushahidi mkubwa zaidi na mkuu zaidi kuliko ushahidi huu? Na haiwezekani kutoa dosari katika ushahidi huu isipokuwa baada ya kutia dosari katika elimu ya Mwenyezi Mungu, na uwezo wake na hekima yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu kujulisha kuhusu ushahidi wa Malaika juu ya yale yaliyoteremshwa kwa Mtume wake, ni kwa sababu ya ukamilifu wa imani yao na utukufu wa hiki kilichoshuhudiwa. Kwani mambo makubwa hawayashuhudii isipokuwa walio maalum. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema katika kushuhudia juu ya tauhidi. "Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye elimu walishuhudia kuwa hakika hapana mungu isipokuwa Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu, Mwenye hekima." "Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi."