Az-Zumar
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ ٱلَّيْلَ عَلَى ٱلنَّهَارِ وَيُكَوِّرُ ٱلنَّهَارَ عَلَى ٱلَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِى لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْغَفَّـٰرُ 5
{5} Mwenyezi Mungu anatujulisha kwamba: "Aliumba mbingu na ardhi" kwa hekima na masilahi, na ili awaamrishe na kuwakataza waja, awalipe mazuri na awaadhibu. "Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku." Kwani viwili hivyo haviwezi kukutana wakati mmoja, bali kikija kimoja katika hivyo, hicho kingine kinatoweka. "Na amelitiisha jua na mwezi." Alijitenga na mamlaka yake, na “akalitiisha jua na mwezi." Vyote viko katika nidhamu iliyoratibiwa vizuri sana. "Kila kimojapo;" yaani, jua na mwezi, "kinakwenda kwa kipindi kilichowekewa" ambacho ni mwisho wa nyumba hii na wakati itakapoharibiwa. Hapo Mwenyezi Mungu ataharibu mitambo yake, jua lake na mwezi wake. Na atawaanzisha viumbe uumbaji mpya, ili wakae na kutulia katika nyumba ya kubakia; katika Bustani za mbinguni au Motoni. "Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu" ambaye hawezi kushindwa, ambaye alishinda kila kitu, ambaye hakuna linaloshindikana kwake, ambaye kutokana na nguvu zake aliviumba viumbe hivi vikubwa na akavitiisha, vikakwenda kwa amri yake. "Mwenye kusamehe mno" dhambi za waja wake waumini waliotubu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Na hakika Mimi ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka." Nami ni Mwenye kusamehe mno mwenye kunishirikisha baada ya kuziona Ishara zangu kubwa, kisha akatubia na kurejea kwangu.