U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Aal-i-Imraan
Suuradda 3

Aal-i-Imraan

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 134

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ فِى ٱلسَّرَّآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَٱلْكَـٰظِمِينَ ٱلْغَيْظَ وَٱلْعَافِينَ عَنِ ٱلنَّاسِ ۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ 134

{134} Kisha akatoa maelezo kuhusu wachamungu na matendo yao, akasema. “Wale ambao hutoa katika nyakati nzuri na nyakati mbaya.” Yani katika hali ya ugumu wao na wepesi wao. Wakiwa katika hali nzuri, hutoa kwa wingi, na wakiwa katika hali ngumu, hawadharau kitu katika mema, hata kama ni kidogo. “Na wanajizuia ghadhabu.” Yani, wanapoudhiwa na wengine maudhi yanayosababisha kuwa na ghadhabu kwao, ambayo ni kuzijaza nyoyo zao hasira zinazolazimu kulipiza kisasi kwa kauli na vitendo. Watu hawa hawatendi kulingana na maumbile ya kibinadamu. Lakini badala yake huzuilia yale yaliyo ndani ya mioyo ya hasira, na huvumilia kukabiliana na wale wanaowaudhi. “Na wanaowasamehe watu.” Na inaingia katika kuwasamehe watu kumsamehe kila aliyekufanyia ubaya kwa kauli au kitendo. Na kusamehe ni bora zaidi kuliko kujizuilia ghadhabu. Kwa sababu, kusamehe ni kuacha kuchukulia ubaya pamoja na kumwachilia mbali aliyefanya ubaya. “Na wanaowasamehe watu.” Na inaingia katika kuwasamehe watu kumsamehe kila aliyekufanyia ubaya kwa kauli au kitendo. Na kusamehe ni bora zaidi kuliko kujizuilia ghadhabu. Kwa sababu, kusamehe ni kuacha kuchukulia ubaya pamoja na kumwachilia mbali aliyefanya ubaya. Na hii huwa tu kwa yule ambaye amejipamba kwa tabia nzuri na akaziacha tabia mbovu, miongoni mwa wale wanaofanya biashara na Mwenyezi Mungu. Na wanawasamehe waja wa Mwenyezi Mungu ili kuwarehemu na kuwafanyia wema, na kuchukia wapatwe na mabaya. Na ili Mwenyezi Mungu amsamehe na malipo yake yawe kwa Mola wake Mlezi Mkarimu, na siyo kwa mja fakiri, kama alivyosema Yeye Mtukufu. “Na mwenye kusamehe na akatengenea, basi malipo yake ni kwa Mwenyezi Mungu.” Kisha akataja hali iliyo ya jumla zaidi kuliko nyingine, na bora zaidi, na ya juu zaidi, na tukufu zaidi, nayo ni ihsan (wema). Yeye Mtukufu alisema, “Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsan (wema)”. Nayo ihsan ni aina mbili: Ihsan katika kumuabudu Muumba, na ihsan kwa viumbe. Na Ihsan katika kumuabudu Muumba iliielezwa na Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa kauli yake. “Ni kwamba umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona. Na ikiwa hamuoni, basi Yeye kwa hakika anakuona.” Na ama ihsan kwa kiumbe ni kuwafikishia manufaa ya kidini na kidunia na kuwaondolea maovu ya kidini na kidunia. Kwa hivyo inaingia katika hilo kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na kuwafunza wasiojua wao. Na kuwapa mawaidha walioghafilika wao, na kuwapa nasiha watu wao wa kawaida na wale wao walio mahususi. Na kujitahidi katika kuunganisha neno lao, na kuwafikishia sadaka na matumizi ya lazima na ya kupendekezwa kulingana na hali zao tofauti tofauti, na sifa zao mbalimbali. Kwa hivyo, inaingia ndani ya hilo kutoa kwa ukarimu, na kuzuia madhara, na kuvumilia madhara, kama vile Mwenyezi Mungu alivyowaeleza wachamungu katika aya hizi. Kwa hivyo, mwenye kufanya mambo haya, basi atakuwa ametekeleza haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya waja wake.