U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Furqaan
Suuradda 25

Al-Furqaan

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 74

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَٰجِنَا وَذُرِّيَّـٰتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَٱجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا 74

{74} "Na wale wanaosema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu." Yaani, wenza wetu, masahabu wetu na wake zetu, "na wana wetu yaburudishayo macho." Na tunapozichunguza hali zao na sifa zao, tunajua vyema wasiwasi wao na cheo chao cha juu [kwamba hayatulii macho yao mpaka wawaone wakimtii Mola wao Mlezi, huku ni wenye kujua na kutenda matendo mema. Na hii kama vile ni dua kwa wake zao] na dhuria wao kwamba watengenee, pia ni dua kwao wenyewe. Kwa sababu manufaa yake yanawarudia wenyewe, na ndiyo sababu wakalifanya hilo kuwa tunu kwao. Wakasema, "Tutunuku" bali dua yao hii manufaa yake yanawarudia Waislamu wote. Kwa sababu kutengenea kwa hao waliotajwa ni sababu ya kutengenea kwa wengi sana yanaofungamana nao na kunufaika nao. "Na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamungu" Yaani, ewe Mola wetu Mlezi tufikishe katika kiwango hiki cha juu, kiwango cha wakweli mno, na wakamilifu miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu. Nacho ni kiwango cha maimamu katika dini, na kuwa mfano mzuri kwa wachamungu katika maneno yao na vitendo vyao, ambao wanafuatwa katika vitendo vyao, na watu wanatulia kwa maneno yao, na watu wema wanatembea nyuma yao, ili waongozwe na waongoke. Na inavojulikana ni kwamba kuomba kufikia kitu, pia ni kuomba kile ambacho hakiwezekani hicho kinachoombwa isipokuwa kwacho. Na kiwango hiki - kiwango cha uimamu katika dini - hukitimii isipokuwa kwa uvumilivu na kuwa na yakini, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanaoongoza watu kwa amri yetu, waliposubiri na wakawa na yakini na Ishara zetu." Basi dua hii inalazimu matendo na uvumilivu juu ya kumtii Mwenyezi Mungu na dhidi ya kumuasi na juu ya majaliwa yake machungu, na kuwa na elimu kamili ambayo inamfikisha mwenyewe katika daraja ya yakini, hayo ni heri nyingi na kipawa kikubwa, na kwamba wawe katika viwango vya juu iwezekanavyo vya maadili mema baada ya Mitume.