An-Noor
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱلطَّيْرُ صَـٰٓفَّـٰتٍ ۖ كُلٌّ قَدْ عَلِمَ صَلَاتَهُۥ وَتَسْبِيحَهُۥ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِمَا يَفْعَلُونَ 41
{41} Mwenyezi Mungu aliwaonya waja wake juu ya ukuu wake na ukamilifu wa mamlaka yake na kufukarika kwa viumbe wote kwake katika ubwana wake na ibada zake; akasema, ''Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa vilivyomo katika mbingu na ardhi.'' Wanyama na vitu visivyo na uhai, ''na ndege wakikunjua mbawa zao;'' yaani, wakikunjua mbawa zao katika anga la mbingu wanamsifu Mola wao Mlezi. "Kila mmoja,'' kati ya viumbe hawa, ''amekwisha jua Swala yake na namna ya kumtakasa kwake.'' Yaani, kila mmoja ana swala na ibada kulingana na hali yake sahihi, na Mwenyezi Mungu amempa msukumo kwa sala hiyo na sifa: aidha kwa njia ya wajumbe kama Majini, wanadamu na Malaika, au kwa msukumo kutoka Kwake kama viumbe wengine wote na wengineo. Uwezekano huu una nguvu zaidi kutokana na dalili ya kauli yake isemayo, ''Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyafanya;'' yaani, anajua matendo yake yote, basi hakuna kilichofichika kwake, na atawalipa kwa hayo. Na atakuwa kwa hilo, ameunganisha elimu yake kwa matendo yao, kupitia mafundisho yake, na elimu yake inayojumuisha malipo. Inawezekana kwamba kiwakilishi katika usemi wake: “amekwisha jua Sala yake na namna ya kumtakasa kwake,” kinamrejelea Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alijua ibada zao, hata kama nyinyi enyi waja hamkuwa mkizijua isipokuwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwako. Aya hii ni kama Mwenyezi Mungu anavyosema: "Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira."