Al-Anbiyaa
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
أَمِ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ ۖ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِىَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِى ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٱلْحَقَّ ۖ فَهُم مُّعْرِضُونَ 24
{24} Kisha akarudi katika kuikashifu hali ya washirikina, na kwamba walijifanyia miungu pasi na yeye. Basi waambie, kwa kuwakemea na kuwakaripia, "Au wamejifanyia miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu" juu ya usahihi wa kile mnachofanya. Lakini hawatapata njia yoyote ya kulifikia hilo. Bali ushahidi wa kukata ulikwisha simama juu ya ubatili wake. Na ndiyo maana akasema, "Haya ni ukumbusho wa hawa walio pamoja nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu." Yaani, Vitabu na kisheria vilikubaliana juu ya usahihi wa yale niliyowaambia juu ya ubatili wa ushirikina. Kwa hivyo hiki ni kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho ndani yake kuna ukumbusho wa kila kitu kwa ushahidi wake wa kiakili na wa kimaandiko. Na vitabu hivi vyote vilivyotangulia ni hoja na ushahidi juu ya ubatili wa yale niliyosema. Na ilipojulikana kwamba umekwisha wasimamia ushahidi na hoja juu ya yale wanachofanya, ikajulikana kwamba hawakuwa na hoja yoyote, kwa maana hoja ya kukata kuna uhakika kwamba haina chochote cha kuipinga. Vinginevyo, basi haingekuwa ya kukata. Lakini hata kama kuna chochote cha kuipinga, hayo yote ni fikira potovu tu ambazo haziwezi kusaidia chochote mbele ya haki. Na kauli yake, "Lakini wengi wao hawaijui haki" na walidumu juu ya hayo wayafanyayo kwa kuwaiga watangulizi wao. Wakawa wanajadili bila ya elimu yoyote wala uwongofu. Na hawana tena kutojua kwao haki si kwa sababu ya kufichikana kwake na kutokuwa kwake wazi. Bali ni kwa sababu ya kuipa kwao mgongo. Vinginevyo, ikiwa wangeigeukia hata kwa uchache tu, ingewabainikia haki kutokana na batili kwa njia bainifu na wazi sana. Na ndiyo maana akasema, "kwa hivyo wanapeana mgongo."